Wanamuziki
kutoka Nigeria, Paul Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa
habari (hawako pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi.
Novemba 23 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa
pili kulia ni Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square,
wakiwa na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady
Jay Dee mmoja wa wasanii watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
Mkuu
wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono
na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati
walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu
wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es
Salaam.
MSANII Peter
Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu
wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto jijini Dar es Salaam. Wa kwa
nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na Mjumbe
wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni mfanyakazi wa
Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini waliofanikisha
wasanii hao kutua nchini.
Wasanii
wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto
mwenye ulemavu wa Usonji, Erick wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda
kushiriki kutoa msaada kwa kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni
mwalimu mkuu wa shule hiyo Reuben Gadi na kulia ni Mkuu wa kitengo cha
Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine
wa kampuni hiyo.
Wasanii
wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye
ulemavu wa usonji wa kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya
Mwakifulefule akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa
shule hiyo wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Wasanii
Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule
wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji wa shule ya msingi ya
Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho
kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
***********************************************************
· Waomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini
· Kufanya onesho kwa masaa mawili mfululizo
· Washiriki katika shughuli za kijamii
Baada
ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye
maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa vyombo vya habari nchini
kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama
vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika
Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja
vya Leaders Club.
Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika katika hotel ya Hyatt jijini Dar wasanii hao wamesema
wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata kutoka kwa jamii ya Watanzania
na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi burudani ya kipekee kwa
Watanzania.
Peter Okoye ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo
vya habari vina mchango mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito
kwa vyombo hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
“Vyombo
vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na
kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa
nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze
kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii
kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini
kwao, alisema Paul.
Paul Okoye ambaye ni kaka kwa Peter amesema
“Tumefurahishwa sana na mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi
kufikia sasa, tumejisikia faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu
wake ni wakarimu sana sifa hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na
tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi Mashabiki wetu kufanya Shoo ya
uhakika., alisema Paul Okoye.
Kwa
upande wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,alisema wamejisikia faraja kwa
pamoja kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania
na kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile
kutoa msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia
mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom” Vodacom Foundation”.
“Kwa
upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika kuanzia, masuala
ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na mambo mengine
tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho litaanza saa 1 na
kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na kujiepusha na
vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Wasanii
kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni pamoja na
wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja
na Ben Pol.
Wakati
huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom
Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto
wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini Dar es
Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuwasaidia
watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa kwa wote.