Friday, November 15, 2013


 
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ akiwa stejini. NCHI yetu imejaaliwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji karibu katika kila nyanja. Wapo waliojaaliwa kupewa na hawajui kuvitumia pasipo mwongozo, lakini wengine wanajua kuvitumia na kujiongoza.   Shilole akijiachia stejini na shabiki. Katika Bongo Fleva na Filamu, fani zinazokimbiliwa zaidi na vijana, lipo kundi kubwa la watu wanaotoka kimaisha kupitia huko. Na mmoja wa vijana wenye vipaji, ni Zuwena Mohamed, ambaye mashabiki wa muziki wanamtambua kama Shilole.
Niwe mkweli, simfahamu msichana huyu kwa maana ya kuwahi kufanya naye kazi, ila nimewahi kusikia kazi zake hasa wimbo wake huu unaotamba sasa, Nakomaa na Jiji.
Pamoja na kwamba bado ni msanii mchanga, lakini ameonyesha kuwa anaweza ubunifu. Wengi wanapenda kuimba, lakini waimbe vipi ndiyo huwa tatizo. Ni kama Snura alivyojishauri na kuamua kuipa kisogo fani ya uigizaji na kujikita kwenye mduara. Lakini ndani ya fani, Shilole ni aina ya binti anayewakilisha mastaa uchwara wa kike Bongo, wasiojitambua na bahati mbaya, hatambui hata mahitaji ya wateja wake. Nimewahi kuona mara kadhaa akiandikwa magazetini kuhusu mambo yake mengi yanayokera, hasa aina ya uvaaji. Moja ya jambo lililonitatiza, ni jinsi wakati mwingine anavyovaa blauzi zake tata, zinazoruhusu matiti yake karibu yote kuwa nje!
Lakini nimejikuta nikisita kukaa kimya baada ya kukutana na kauli yake katika moja ya magazeti ya kila siku nchini, akidai kwamba anavaa vile ambavyo watu wamekuwa wakimlalamikia, kwa sababu mashabiki wake ndiyo wanapenda!
Yaani anavyovaa nguo za ajabu ajabu, yaani zenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake hadharani, ndivyo ambavyo watu wanaofurika katika majukwaa anayoimba wanavyopenda.
Ni kweli kwamba katika biashara, ni jambo la msingi sana kutazama nini mahitaji ya wateja. Muziki ni biashara na mashabiki ndiyo wateja wenyewe. Sitaki kuamini kama wale watu wanaojitokeza katika matamasha ambayo Shilole hualikwa kutumbuiza wanafurahishwa nayo.
Kwanza ni jambo la msingi kumfahamisha Shilole kwamba hana mashabiki. Nasema hivi kwa sababu kama leo hii mtu atajitokeza na kuandaa shoo ya mtu mmoja tu, ambaye ni yeye, sidhani kama atafanikiwa. Na katika hili, kuna watu wachache sana wanaweza kujaza watu katika nchi hii, wakiongozwa na Nasib Abdul ‘Diamond’. Shilole anaalikwa katika matamasha kwa ajili ya kuchanganya ladha tu na wala asije akaona watu wanavyopiga kelele anapokuwa jukwaani basi wanashangilia mavazi yake. Huwezi jua, huenda huwa wanamzomea!
Kuvaa ovyo hakuwezi kuwafanya watu waupende muziki wako. Sijawahi kumuona msanii wa kike mvaa ovyo aliyefanikiwa kuuza sana nakala zake katika Tanzania tokea nianze kufuatilia Bongo Fleva. Sana naona wanashindwa tu, wakiongozwa na Ray C!
Lakini kuna wasanii wengi tu wa kike waliofanya vizuri na kujilundikia mashabiki, lakini bado wanavaa mavazi ya heshima jukwaani, kwenye video zao na hata wanapokuwa kwenye matukio ya kijamii. Hapa upo mfano wa Lady Jay Dee kwani ndiye msanii wa kike mwenye mafanikio zaidi lakini anayejiheshimu. Kwangu, kuvaa mavazi yenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili ni kutojiamini. Anataka watu wavutike kwa kuangalia mwili badala ya kazi. Ndiyo hawa hawa waliojazana katika Muvi zetu, wanavaa nusu uchi kuwachota watu akili ili concentration yao iwe kwenye miili yao badala ya kazi zao! Tubadilike. Nimesema mara kwa mara, ukishakuwa staa, unapaswa kuwa mfano ulio bora!

Baada ya Nigeria kuongoza kwa baadhi ya watu wake wengi kumiliki magari ya bei mbaya, sasa kenya wasema kua nao hawapo nyuma. Nimebahatika kuipata picha ya gari aina ya Aston Martin DB 9 yenye thamani ya $300,000 za kimarekaniau milioni 483 za kibongo. Bado haijajulikana gari hiyo hasa inamilikiwa na nani lakini imeonekana ikikatiza mitaa ya nairobi,
MWIGIZAJI wa Filamu Bongo Dianarose kimaro ‘Diana’ ametamba kwa kusema kuwa amekamilika katika tasnia ya filamu na hakuna mwigizaji wa kike ambaye anamfikia kwa kiwango alicho nacho katika uigizaji kwani kila akiwangalia wanaigiza kawaida na hajaona mpinzani wake wa kweli katika fani hiyoSwahiliwood kwa sasa.
Dianarose Kimaro
Diana aka Sikujua mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

diana 555Nilipokuwa shule nilijitenga na sanaa sasa nimerudi watasubiri kwa upande wa wasanii wa kike wanaigiza kwa kiwango cha chini, au kwa kutopewa nafasi wanazomudu kuna watu wanajua mimi na Lulu ni mapacha lakini kwa filamu niliyoifanya hivi karibuni ya Kigodoro shoga yangu atasubiri,”anasema Diana.
Diana ambaye mara nyingi ushirikiana na Lulu kataika filamu kwenye uigizaji sasa anasema ameamua kusimama yeye kama yeye na anawahakikishia kuwa wapenzi wa filamu kuwa wasubiri filamu inayokuja ya ‘Kigodoro Kanitangaze’ambayo kaigiza kama mhusika akitamba kuwa yeye ni kiboko yao rika lake lote anawafunika.

Dianarose Kimaro







WAKATI filamu nyingi za bongo bajeti yake si ile ya kushtua mtu kama kazi za wasanii wa mbele, na kwa kulitazama hilo msanii Jackline Wolper ameamua kuweka wazi fungu lake ili kwa wale wanaotaka kumshirikisha kwenye filamu zao basi wajue kuwa anaweza kucheza kuanzia milioni 1 na kuendelea chini ya hapo hapotezi muda.

Wasanii wa Tanzania wanatatizo kubwa la kutotumia pesa ya kutosha katika utengenezaji wa filamu zao, na wengi bajeti zao ni chini ya mil 8, hivyo kwa kiasi anachokitaka Wolper sijui kama ni kweli anaweza kulipwa ingawa wengi tumewazoea wakisema hivyo lakini mwisho wa siku unasikia kacheza filamu kwa laki 2.

Msanii huyo aliweka wazi ishu hiyo wakati akizungumza kwenye mahojiano na televisheni ya Clouds TV kupitia kipindi cha Take One, ambapo aliulizwa kiasi anachotaka kulipwa kucheza filamu, ndipo alipotaja fungu hilo.

“Kwa kweli suala la kulipwa mara nyingi huwa inatengemea na filamu yenyewe lakini kwa upande wangu naweza kusema kwamba kuanzia milioni 1 hapo nafanya kazi,” alisema.
Tuhuma ya mastaa Bongo kujihusisha na mambo ya ulozi au uchawi imeibuliwa upya na safari hii bundi kajikita zaidi kwenye kiwanda cha sinema za Kibongo, Ijumaa lina ripoti kamili.

Jack Wolper.
UCHUNGUZI
Uchunguzi wa gazeti hili ndani ya ulimwengu wa mastaa hao ulibaini kwamba, ukiwaacha wale wa Bongo Fleva ambao wamekuwa wakishikana uchawi kila kukicha, kwenye filamu ndiko hakufai.
Ilibumburuka kwamba masuala ya kurogana ndiyo yamesababisha filamu za baadhi yao kudoda na kukosa soko.
Inaelezwa kwamba mbali na sinema  zao kubuma sokoni pia wamekuwa wakizibiana riziki za tenda kama ilivyokuwa zamani.
Elizabeth Michael 'Lulu'.
KIVIPI?
Kwa mujibu wa ‘mtaalam’ wao mwenye kituo cha kazi huko Yombo-Buza, Dar, wanachokifanya ni kufifisha na kuzimana nyota hivyo kumpotezea mhusika mvuto kwenye jamii.
“Unajua kuna mastaa ambao walikuwa na majina makubwa sana lakini siku hizi siyo kama zamani.
“Baadhi wanawaroga wenzao kwa kuwasababishia matatizo ya magonjwa au kwenye familia,” alisema mmoja wa wasanii waliokuwa waking’ara zamani lakini siku hizi kafifia huku akimtolea mfano mwigizaji mmoja wa kiume ambaye mkewe aliwahi kumkuta na hirizi.
Katika uchunguzi huo, baadhi ya mastaa walikuwa wakinyoosheana vidole wao kwa wao huku listi ndefu ya mastaa wanaokesha kwa waganga kuwamaliza wenzao ikianikwa (majina tunayo).
Ili kupata uthibitisho wa uchunguzi huo, gazeti hili lilizungumza na baadhi ya vinara wa filamu za Kibongo ambapo wengi walikiri kukithiri kwa ushirikina kwenye tasnia hiyo.
JACOB STEVEN ‘JB’: Sanaa yoyote ili idumu muda mrefu inahitaji baraka na neema ya Mungu. Sisi tulianza enzi za Nyota Ensemble ‘Mambo Hayo’, baadaye ilikuja Kaole Sanaa Group ndipo kukaibuka mapinduzi sisi tukashuka.
Mimi siamini mambo ya uchawi ila naamini katika kazi tu, wasanii waache kufanya kazi kimazoea.
Masuala ya kurogana mimi spendi kuyapa nafasi maana hayo kila sehemu yapo, ninachoweza kusema ni kwamba wasanii wengi wa Bongo hawapo ‘siriasi’.
JACQUELINE WOLPER: Mimi naamini sana katika kazi lakini kwa kuwa Mungu ndiye kanipa jina hili, sina budi kumshukuru yeye ila kama nimelipata kwa njia ya uganga basi nikose kabisa.
ROSE NDAUKA: Uchawi ni ishu inayonisikitisha sana na ukweli wapo mastaa wanafanya mambo hayo ili wapande. Mimi najua Mungu hawezi kuwasaidia so nawashauri wafanye kazi, wasihangaike na uchawi kwa sababu hauwezi kuwapandisha.
KAJALA MASANJA: Kusema kweli uchawi unatajwa sana kwenye tasnia ya filamu Bongo hadi inanifanya kuamini hivyo kwa sababu kuna watu kweli wakikuona unang’ara kwenye muvi watafanya kila wawezavyo ili wakushushe tu na hasa kwa njia ya ushirikina.
SINGLE MTAMBALIKE ‘RICHIE’: Mimi asili yangu ni Mwanza so kama ujuavyo watu wa Mwanza ni wachapa kazi, so nipo makini sana na kazi yangu ya filamu na nipo kwenye tasnia kwa miaka 17 na maisha yangu nayafanya ya kawaida tu wala sipendi kujikweza sana.
Kwa staili hiyo ningetumia nguvu za giza ningekuwa tajiri namba moja  hapa nchini maana siri ya kazi yoyote ni kuiheshimu na kujibidiisha.
ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’: Tasnia yetu ya filamu naona kama hatuangalii mbali maana kwa wenzetu wanashindana kikazi na si uchawi kama huku wanaofikiria kuwashusha wenzao kisa wanaona wanafanya vyema, mimi ninachoweza kusema watu wafanye kazi na wasibaki kuangalia nani anafanya nini na kumfanyia mambo kama hayo yasiojenga maisha.
RUTH SUKA ‘MAINDA’: Mimi sijui sana kama kuna watu wanafanya ushirikina. Ninachowaomba wamtegemee sana Mungu kwani ninachoamini mimi kila kitu kipo kwa makusudi ya Mungu. Kama ukimroga mwenzio ili ashuke basi hata wewe huwezi kufika mbali.
JACQUELINE PENTZEL ‘JACK CHUZ’: Kweli mimi ninaumizwa sana na watu wanaotumia uchawi kuzima nyota yangu kwa sababu kweli wapo wanaofanya hivyo tunawaona hata huko lokesheni wanakamatwa na hirizi.
Wengine wanakutwa na matunguri ila mwisho wa siku naomba wajue kuwa nyota na mafanikio ya mtu huletwa na Mungu na kujibidisha katika kazi hivyo ninachoweza kuwashauri watu kama hao waachane na imani za kishirikina.
SALUM HAJI ‘MBOTO’: Mimi ninachojua watu wanatengeneza muvi kupitia migongo ya wenzao, unakuta mtu anatengeneza sinema lakini anajua kabisa bila kumchezesha fulani hawezi kuuza hivyo anatumia nyota ya mwenzake kuuza filamu yake.
AUNT EZEKIEL: Siamini sana katika kurogana ila wanotumia njia hizo siamini kama wanafanikiwa kiasi hicho maana uigizaji ni kipaji kutoka kwa Mungu na hakuna awezae kushusha kipaji hicho ila najua uchawi upo na watu wanatumia uchawi kwenye mambo yao.
STEVE NYERERE: Uchawi haupo kwenye filamu tu hayo yapo hata kwenye siasa. Watu kibao wanatembelea nyota za watu. Wapo wanaoshinda kwa waganga, tunawajua ila cha msingi wafahamu kuwa hata ukimfanyia mtu kitu gani huwezi kuwa staa.
SALOME NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’: Mimi ninaona kama chalenji tu na kinyongo, maana wengi wanaotumia nguvu za giza hawachukui muda mrefu wanashuka wao. Ninachoona mimi waachane na nguvu za giza wamtegemee Mungu.
Baadhi ya waigizaji wengine waliowahi kurogwa na wenzao ni pamoja na Wema Sepetu, Blandina Chagula ‘Johari’, Nuru Nassor ‘Nora’ na wengineo.
At 17, Julia Montes is the proud owner of a new two-story home in Antipolo City. She never expected to be able to buy her own house at such a young age. And she’s excited to sleep in a bedroom of her own!
She and her family will move to the new house in April.
“I used to share a room with my four siblings. I would get so stressed out whenever the room was in disarray,” Julia tells Living Stars. “My new room has lots of storage space. I don’t like clutter. I hate not finding stuff when I need them.”
Julia first appeared in the youth-oriented programs “Goin’ Bulilit” and “Growing Up,” before she was cast to play the lead in the top-rated 2010 drama series “Mara Clara.” She currently portrays the heroine Katerina Alcantara-Montenegro on ABS-CBN’s latest hit show “Walang Hanggan.”
Julia says she and Katerina are alike in that they both value family: “We’re both scared of losing our loved ones and of being alone. But unlike Katerina, I don’t give up easily. I fight for what I want. I work hard to fulfill my dreams.”
forward look
Julia was born Mara Hautea Schnittka to a Filipino mother, Gemma Hautea, and a German father, Martin Schnittka, in Pandacan, Manila. Julia’s dad left them when she was a baby, and only her deaf mother raised her with the help of her grandmother Flory. In 2011, Julia finished high school with good grades at the Blessed Hope Christian School. She is now the family breadwinner.
Accessories
“Less is more,” Julia stresses. “Collect classic pieces—simple stud earrings, bangles and watches, and dress your age. Belts are often neglected, but a belt can transform your V-neck
“LESS is more,” says the practical teen. Julia wears gladiator sandals by Michael Antonio and floral overalls from HerBench.
shirt from simple to chic.”
Julia says her favorite pair of Ray-Ban Aviator shades is a gift from Lino Cayetano, director of “Growing Up.”
Book
She received the book “What Matters Most for Teens” from Linggit Tan, ABS-CBN head for TV entertainment production. “Tita Linggit always reminds me to keep my feet planted firmly on the ground,” she said.
Gadgets
“I’m a MyPhone endorser,” Julia says. “I use its T18 Duo. It’s small and perfect for students. I also have a MyPhone with a built-in TV. Another phone I like is adorned with Swarovski crystals. It’s perfect for formal events.”
“You don’t need expensive gadgets,” Julia points out. “Go for quality and function. Make sure to read reviews about a particular item before getting it. There are pieces that may look attractive on the outside, but looks can deceive.”
Scents
Julia is turned off by colognes with strong scents. “I like Fire by Boardwalk. I also like Bulgari because it’s a perfume that I can use every day. I prefer scents that are powdery, sometimes floral,” she says.
Shoes
“I love shoes! I probably have over 20 pairs right now,” she beams. “I use all of them. I had shelves built just for my shoes in my walk-in closet at home.”
SHE SAYS she can’t wait to display her toy collection in her new home.
“This pair of fuchsia high-heeled pumps from Michael Antonio is fabulous,” she says. “People were worried that it was too high but I’m used to wearing five-and-six-inch heels.”
Julia also likes Skechers sneakers. “They’re light and comfortable to use and I can easily match them with any workout clothes.”
she also own a solon
Makeup
“This lip palette from Krayola has different colors that you can mix and match. Just use a good lip brush,” she says. “I prefer flesh or old rose for my lips, since I believe that less is more. I advise teenagers to stick to lip balm. It’s not good to wear lip color every day at a young age. I only have a lot because of work.”
She is obsessed with makeup more than with shoes. “I used to dream of becoming a makeup artist,” Julia says. “I’ve been experimenting on makeup since I was 9! I do my own face. I read magazines or surf the Net for the latest styles and techniques.”
“You don’t need expensive makeup, especially if you’re a teenager and can’t afford it,” says the practical buyer. “Plus, some cosmetics are harsh on young skin.”
Clothes
“I’m an endorser of HerBench. Their clothes are versatile,” she explains. “Take this plain cotton shirt for example. I can use it to the gym, but I can also wear it with a skirt and transform it into something really girly. This gray printed shirt is good for going out with friends, but with the right accessories you can turn it into a costume for a production number on TV.”
“This white lacy blouse has a romantic look. It’s also easy to match with other outfits because it has the most basic cut and color.
“This off-shoulder blouse from Forever 21 is very sexy. It shows just enough skin. I can use this with a skirt or a pair of shorts,” the actress says.
A PAIR of stylish earrings, perfect for either casual or formal events
Julia is into maxi-dresses lately because they’re comfortable yet classy. “This long blue-green skirt can go with flats or high-heeled shoes,” she points out.
Bag
“This brown leather bag is my favorite. Its color is easy to match and it’s big enough to carry all my stuff. I’m a girl scout—ready with everything, including alcohol and medicines,” Julia says.
Toys
Her stuffed pink toy pig was a Christmas present from her supporters, Julia’s Angels. “Most of the stuffed toys I have are gifts,” she said.

waliotembelea blog