Thursday, April 2, 2015



Morocco2015


‘Morocco ilikjuwa imefungiwa na CAF kushiriki AFCON mbili zijazo baada ya kujitoa kuandaa AFCON iliyopita kwa hofu ya mlipuko wa Ebola.’
Usiyempenda kaja! Ndivyo unaweza kusema baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Kimataifa (CAS) kutengua hukumu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuifungia Morocco kushriki AFCON mbili zijazo 2017 na 2019.
CAF iliifungia nchi hiyo ya kifalme kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya timu za taifa barani kutokana na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) kujitoa kuandaa fainali za mwaka huu za Afrika ambazo baadaye zilifanyika Guinea.
Mbali na kifungo hicho, CAF pia iliitaka FRMF kulipa faini ya dola za Marekani (US$) milioni 8.7 ambacho CAS imekipunguza hadi 50,000 kwa mujibu wa mtandao wa futaa.com wa Kenya.
Kwa mujibu wa BBC,  CAF ilidai kuwa imeingia hasara kubwa kwa kubadili nchi mwenyeji wa AFCON 2015 kutoka Morocco hadi Equatorial Guinea – ikiwa ni miezi miwili tu kabla ya kuanza kwa michuano yenyewe.
Morocco ilitaka michuano hiyo isogezwe mbele au kusitishwa kutokana na mlipuko wa Ebola ambao ni tishio barani Afrika, lakini ombi lao lilitupiliwa mbali na CAF ambao baadaye wakaitoa timu ya Morocco katika michuano hiyo kabla haijakata rufaa.
Ligi kuu Tanzania Bara itaendelea wikiendi hii huku kocha wa mabingwa wa zamani wa Tanzania Bara, Simba, Mserbia Goran Kopunovic akiipigia mahesabu ya ushindi timu ya Kagera Sugar katika uwanja wa Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga ambao wanautumia kama uwanja wao wa Nyumbani baada ya ule wa Kaitaba kuwa kwenye Matengenezo. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa hapo Jumamosi kesho kutwa.
Katika kile kinachoonekana mpango mzima wa kulipiza kisasi, Kopunovic amesema wachezaji wake wapo imara kuifunga Kagera Sugar katika uwanja wa nyumbani. Kagera Sugar ikiwa na pointi 28, ilifanikiwa kuifunga Simba 1-0 katika mchezo wao uliopita.
Simba ina pointi 32, ikiwa ya tatu katika msimamo, ambapo wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 40 huku Azam wakiwa nafasi ya pili na pointi 36.
Mechi nyingine za Jumamosi ni Coastal Union itakapocheza na Tanzania Prisons mkoa wa Tanga, Kaskazini mwa Tanzania.

unnamed
wachezaji wa Coastal Union wakiwa na
mazoezi jana kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly chini ya
Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu “Julio”,
………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, TANGA
Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu za
wapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua
wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala
salama.Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo
yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini
hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi
wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata
matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka
wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.
Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili
kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo
ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.
Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi
katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa
hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi na (kulia) ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati), ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi (kushoto) na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti wa kampuni hiyo, Gaurav Dhingra wakionyesha ishara dole wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Meneja wa Kitengo cha Huduma za Intaneti, Gaurav Dhingra akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa kampeni kabambe ya Airtel inayotoa ofa ya intaneti bure ijulikanayo kama ‘Na Like asubuhi’, katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampunihiyo jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akifatiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Levi Nyakundi.



LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Aprili 4

14:45 Arsenal vs Liverpool
17:00 Everton vs Southampton
17:00 Leicester vs West Ham
17:00 Man United vs Aston Villa
17:00 Swansea vs Hull
17:00 West Brom vs QPR
19:30 Chelsea vs Stoke

Jumapili Aprili 5

15:30 Burnley vs Tottenham
18:00 Sunderland vs Newcastle
Jumatatu Aprili 6

22:00 Crystal Palace vs Man City
Jumanne Aprili 7
21:45 Aston Villa vs QPR


Jikekizz la nguvu la kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Radio 93.7 EFM.

Mstahiki Meya wa Kinondoni, Yussuf Mwenda akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila walipo kutana katika ofisi za EFM asubuhi ya leo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mtangazaji wa kipindi cha Joto la Asubuhi, Dennis Ssebo akiwa na Mkurugrnzi Mkuu wa Radio 93.7 EFM, Francis Ciza.

Mmoja wa wageni waliotembelea ofisi hiyo, Sukhwinder Bajwa ambaye ni Mkuu wa Masoko kutoka Kampuni ya Zantel, akizungumza wakati wa kuipongeza EFM siku ya leo.

Samira Kiango ambae ni Mhariri Msaidizi pamoja akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EFM, Francis Ciza.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila alipokua akiongea moja kwa moja kutoka katika kituo cha 93.7 EFM siku ya leo.

Ukafika wakati wa kukata keki kwa pamoja.

Meneja Mkuu wa EFM, Geofrey Ndaula, alikipiga stori mbili tatu na Reuben Ndege (Ncha kali) pamoja Sostenas Ambakisye (Rdj-Kamokali).


Picha ya familia yetu.

Keki tayari kwa kuliwa.

Samira Kiango pamoja Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila.


Jumamosi Signal Iduna Park itakuwa na kivumbi kikubwa wakati Wenyeji Borussia Dortmund watakapocheza na Mahasimu wao wakubwa wa Miaka ya hivi karibuni Mabingwa Bayern Munich.
Licha ya kuwa Msimu huu Bayern wanaelekea kuutwaa Ubingwa kilaini wakiwa Pointi 10 mbele kileleni na Dortmund kujikwamua toka mkiani na sasa wako Nafasi ya 10, Mechi hii Siku zote haikosi ushindani.
Hivi karibuni ushindani huu umeongezeka kwa uhasama baada ya Bayern 'kuwapora' Dortmund Mastaa wao Robert Lewandowski na Mario Goetze.
Pengine hali hiyo, ikichanganywa na kukumbwa na Majeruhi kibao, ndio ilisababisha Dortmund kupwelepweta Msimu huu.
Hali hii sasa imewageukia Bayern ambao wana Majeruhi wa Mastaa wao wakubwa, Arjen Robben, ambae ndie Mfungaji wao bora, na David Alaba huku Franck Ribbery akiwa na hatihati kucheza kutokana na maumivu.
www.bukobasports.comBUNDESLIGA
RATIBA
Jumamosi Aprili 4

16:30 Bayer Levkn v Hamburger SV
16:30 Eintracht Frankfurt v Hannover 96
16:30 Sport-Club Freiburg v 1. FC Köln
16:30 SV Werder Bremen v 1. FSV Mainz 05
16:30 TSG 1899 Hoffenheim v Borussia Mönchengladbach
16:40 VfL Wolfsburg v VfB Stuttgart
19:30 Borussia Dortmund v Bayern Munich

Jumapili Aprili 5
16:30 FC Augsburg v Schake
18:30 Hertha BSC v SC Paderborn 07



Msanii mkali wa maigizo na vichekesho, Nchini, Amri Athuman a.k.a King Majuto anatarajiwa kufanya shoo maalum ya vichekesho katika viwanja vya kufurahia watoto Kariakoo, Aprili 7, mwaka huu Mjini Unguja, Zanzibar.
Kwa mujibu wa wandaaji wa shoo hiyo kampuni ya Bond Entertainment Limited, kwa kushirikiana na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), walieleza kuwa gwiji huyo wa vichekesho King Majuto ambaye pia ni mkongwe anayetamba ndani na nje ya Tanzania ataonyesha vichekesho vyake hivyo hiyo Aprili 7, katika mapumziko ya siku ya Karume (KARUME DAY).

“Ni wakati wa familia kujitokeza kwa wingi siku ya Jumanne ya tarehe 7/4/2015, kuja kumshuhudia King Majuto na kufurahia vichekesho vyake” ilieleza taarifa hiyo.

Ambaapo katika siku hiyo ya Aprili 7, kwenye shoo hiyo ya vichekesho, kiingilio kwa wakubwa ni Tsh.2,000/= huku kwa watoto itakuwa ni sh 1,000.

Pichani ni baadhi ya vichekesho vyaa gwiji huyo, King Majuto katika moja ya kazi zake akiwa na msanii Wema Sepetu.
Onyesho hilo lenye vionjo vya “Njoo uvunje mbavu na King Majuto!!. Taarisha mbavu zako” limedhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya tigo Tanzania.
 



Huku kukiwa na habari nzito kuwa Chipukizi huyo moto mwenye Miaka 20 anaechezea pia England yuko mbioni kwenda Real Madrid, Bayern Munich, Manchester City na Arsenal. Liverpool ilitaka haraka kumfunga kwa kumpa Mkataba mpya mnono lakini kambi ya Sterling imegoma.
Mkataba wa sasa wa Sterling na Liverpool unakwisha 2017.

Sterling anahusishwa kwenda katika Klabu kama Real Madrid, Bayern Munich, Manchester City na Arsenal

Sterling ofa ya £100,000 kwa wiki Klabuni Liverpool ameitolea nje!
Kocha Mkuu wa Liverpool Brendan Rodgers itabidi akae kiti kimoja na Sterling iliasaini Mkataba mpya Anfield

Wakazi wa Geita Pasaka hii watapata kuwaona live' Wasanii wa Kikundi mahiri cha KAPOTIVE Star Singers- Bukoba
TAMASHA hilo la PASAKA litafanyika Jumapili tarehe 05/04/2015 sikukuu ya Pasaka yenyewe katika ukumbi wa GEDECO, kuanzia saa 9 mchana hadi 2 usiku.
Kiingilio kwa watu wazima ni kununua tu DVD mpya inayoitwa KAPOTIVE LIVE SHOW kwa Tshs.10,000 tu. DVD hii inacheza pande zote mbili (Two in One). Watoto Tshs. 3,000 tu.
Karibuni sana tusherekee Pasaka kwa shangwe tukiwa na kundi zima la KAPOTIVE Star Singers-Bukoba. Mratibu wa Tamasha hilo Bw. Andrew Kagya akizungumza na Mwandishi wetu amewataka Wakaazi wa Mji wa Geita kuingia kwa Wingi katika Ukumbi huo ili kuburudika kwa Nyimbo za Injili na hapo hapo Mashabiki watajipatia DVD Mpya ya Kikundi hicho chenye makazi yake Mkoani Kagera.
Baadhi ya Waimbaji wa Kikundi cha Kapotive Star Singers wakiimba na kucheza wimbo wa Kihaya ambao ni moja ya Nyimbo zilizopo kwenye DVD hiyo mpya.

waliotembelea blog