Thursday, April 2, 2015

unnamed
wachezaji wa Coastal Union wakiwa na
mazoezi jana kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly chini ya
Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu “Julio”,
………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, TANGA
Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu za
wapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua
wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala
salama.Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo
yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini
hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi
wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata
matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka
wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.
Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili
kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo
ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.
Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi
katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa
hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog