Ligi
kuu Tanzania Bara itaendelea wikiendi hii huku kocha wa mabingwa wa
zamani wa Tanzania Bara, Simba, Mserbia Goran Kopunovic akiipigia
mahesabu ya ushindi timu ya Kagera Sugar katika uwanja wa Uwanja wa CCM
Kambarage Mjini Shinyanga ambao wanautumia kama uwanja wao wa Nyumbani
baada ya ule wa Kaitaba kuwa kwenye Matengenezo. Mchezo huo unatarajiwa
kuchezwa hapo Jumamosi kesho kutwa.
Katika kile kinachoonekana mpango mzima wa kulipiza kisasi, Kopunovic amesema wachezaji wake wapo imara kuifunga Kagera Sugar katika uwanja wa nyumbani. Kagera Sugar ikiwa na pointi 28, ilifanikiwa kuifunga Simba 1-0 katika mchezo wao uliopita.
Simba ina pointi 32, ikiwa ya tatu katika msimamo, ambapo wapinzani wao wa jadi, Yanga wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 40 huku Azam wakiwa nafasi ya pili na pointi 36.Mechi nyingine za Jumamosi ni Coastal Union itakapocheza na Tanzania Prisons mkoa wa Tanga, Kaskazini mwa Tanzania.

0 maoni:
Post a Comment