‘Morocco ilikjuwa imefungiwa na CAF kushiriki AFCON mbili zijazo baada ya kujitoa kuandaa AFCON iliyopita kwa hofu ya mlipuko wa Ebola.’
Usiyempenda kaja! Ndivyo unaweza kusema baada ya Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Kimataifa (CAS) kutengua hukumu ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuifungia Morocco kushriki AFCON mbili zijazo 2017 na 2019.
CAF iliifungia nchi hiyo ya kifalme kushiriki michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya timu za taifa barani kutokana na Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) kujitoa kuandaa fainali za mwaka huu za Afrika ambazo baadaye zilifanyika Guinea.
Mbali na kifungo hicho, CAF pia iliitaka FRMF kulipa faini ya dola za Marekani (US$) milioni 8.7 ambacho CAS imekipunguza hadi 50,000 kwa mujibu wa mtandao wa futaa.com wa Kenya.
Kwa mujibu wa BBC, CAF ilidai kuwa imeingia hasara kubwa kwa kubadili nchi mwenyeji wa AFCON 2015 kutoka Morocco hadi Equatorial Guinea – ikiwa ni miezi miwili tu kabla ya kuanza kwa michuano yenyewe.
Morocco ilitaka michuano hiyo isogezwe mbele au kusitishwa kutokana na mlipuko wa Ebola ambao ni tishio barani Afrika, lakini ombi lao lilitupiliwa mbali na CAF ambao baadaye wakaitoa timu ya Morocco katika michuano hiyo kabla haijakata rufaa.
0 maoni:
Post a Comment