Monday, July 15, 2013


Ray mtayarishaji na muongozaji wa filamu Swahiliwood.
MWIGIZAJI, mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi ‘Ray the Greatest’ hivi karibuni aliangusha bonge la sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuwakaribishwa rafiki zake na wadau wa filamu katika moja ya Hotel, siku hiyo pia aliweza kumkumbuka swahiba yake marehemu Kanumba na kuhisi uenda angekuwepo siku hiyo.
. “Ni siku ambayo nimesheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zangu wa karibu na wasanii wenzangu, ni siku ambayo nimekumbuka mambo mengi sana katika maisha yangu, mara nyingi swahiba wangu marehemu Kanumba siku kama ya leo ningekuwa naye katika sherehe kama hii, lakin ndio mambo ya Mungu huwezi kulaumu kilichobaki ni kumuombea Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani Amen,” alisema The Greatest.

Steven Kanumba, Vincent KigosiMaswahiba wawili wakitoka safari marehemu Kanumba na Ray
Vincent Kigosi, InnoRay akiwa na mdau wa filamu Inno.
Katika sherehe hiyo iliyopambwa na vinywaji na malaji kibao ilijumuisha wasanii nguli katika tasnia ya filamu kama Bonge la bwana, JB, Maya, Odama, Chikoka na wasanii wengine kibao huku kukiwa na michezo kadha wa kadhaa ni jambo jema kwa marafiki kukumbuka katika matukio kama hayo.
.

Vincent Kigosi, steven kanumbaRay akiwa na marehemu katika filamu ya Oprah
Pengine sasa watu wanaona tasnia ya filamu kupwaya baada ya Ray kukosa mpinzani wa kweli katika tasnia ya filamu, tofauti na alivyokuwepo marehemu Kanumba ushindani wa mafanikio ulikuwa wazi kuanzia ubora wa kazi na umiliki wa mali ikiwa sambamba na magari mazuri, vifaa vya Production jambo ambalo kwa sasa analifanya Ray pekee hana mpinzani

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog