Alizaliwa Juni 24 1987 Rosario Argentina baba yake Jorge Horacio Messi alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha chuma Argentina na mama yake Celia MarÃa Cuccittini alikuwa msafishaji.
Akiwa na umri wa miaka mitano Messi alianza kucheza soka katika klabu ya Grandoli ya mtaani kwao ambapo kocha wa timu hiyo alikuwa baba yake.
Mwaka 1995 Messi alijiunga katika timu ya vijana ya Newell’s Old Boys ambayo ndani ya miaka minne ilipoteza mechi moja pekee, akiwa na umri wa miaka 11 Messi
alipata matatizo ya ukuaji, ugonjwa ambao ulikuwa unagharimu matibabu
dola 900 kwa mwezi ambayo ni zaidi ya Tsh 1900,000/= kiasi ambacho klabu
na familia yake hawakuwa na uwezo wa kugharamia.
Mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona wakati huo Carles Rexach akakubali kukiokoa kipaji cha Messi na kumchukua Messi pamoja na baba yake ili akamuangalie Messi wakati anapatiwa matibabu Barcelona alijiunga La Masia kituo cha kukuzia vipaji vya soka kinachomilikiwa FC Barcelona.
2. Ricardo Kaka
Ricardo Kaka hakuwa tofauti sana na vijana au watoto wengi wa Afrika
ambao huwa na tabia ya kujifunza vitu tofauti tofauti wakati wakiwa
wadogo, licha ya kuwa hakutokea katika familia yenye maisha magumu,
kipindi ana umri wa miaka 8 aliwahi kucheza tennis kabla ya kuamua
kujikita katika soka.
Kaka baba
yake alikuwa engeneer na mama yake alikuwa mwalimu kwa hiyo suala la
fedha kwao haikuwa tatizo kitu kilichomfanya aweze kumudu kupata elimu
na kucheza soka… Uwezo wake wa soka ulianza kuonekana akiwa na miaka 15
wakati ambao alikuwa akiichezea timu ya shule ya Alphaville ndipo klabu ya Sao Paulo ilipomuona na kumpa nafasi ya kujiunga katika Academy ya Sao Paulo.
Alipokuwa na umri wa miaka 18 Kaka
alipata mkasa ambao huenda ungeweza msababishia kuachana na soka baada
ya kupata ajali wakati akiwa anaogelea katika swimming pool na
kusababisha tatizo katika uti wa mgongo kitu ambacho kingeweza kupelekea
apate ugonjwa wa kupooza.
3. Mario Balotelli
Jina lake kamili ni Mario Barwuah raia wa Italia, wazazi wake ni wahamiaji kutokea Ghana, wakati ana umri wa miaka mitatu wazazi wake walishindwa kumtunza na kumtoa katika familia ya kizungu ya Francesco Balotelli na mkewe Silvia wamlee hapo ndipo alipolipata jina lake la Balotelli.
Balotelli
aliwahi kuwalaumu wazazi wake wa kumzaa kuwa walimtelekeza licha ya
kuambiwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kumtunza, kazaliwa na kukulia Italia ila kutokana na asili ya wazazi wake Balotelli alikuwa na uwezo wa kuichezea timu ya taifa ya Ghana kabla ya mwaka 2008 kupewa uraia wa Italia na kutangaza kuwa yeye ni muitaliano.
“Mimi ni muitalia, naipenda Italia na siku zote nitacheza timu ya taifa ya Italia”>>>Mario Balotelli
0 maoni:
Post a Comment