ARSENE Wenger amewalaumu wachezaji wake
kwa kushindwa kuonesha kiwango kizuri baada ya kufunbgwa 2-0 na Borrusia
Dortmund katika mchezo wa ligi ya mabingwa jana usiku (Uefa), huku
wakirudi nyumbani na balaa kufuatia mkali wao Jack Wilshere kupata
majeruhi.
Wilshere alitegua kifundo chake cha mguu
wa kulia katika dakika za majeruhi na Wenger amekiri kuwa ameumia
sehemu ile ile ambayo ilimuweka nje ya uwanja kwa miezi 17.
"Ni vigumu sana kusema jinsi ilivyo
mbaya," alisema kocha wa Arsenal. "Kwa kawaida isingekuwa mbaya sana ,
lakini nina wasiwasi kidogo kutokana na historia yake".
Jack Wilshere akianguka chini dakika za
mwisho na kupata majeruhi iliyomchanganya Wenger ambaye ana matatizo
hayo katika kikosi chake
Jack Wilshere ameumia kifundo cha mguu wa kulia kilichomsumbia miaka miwili iliyopita
"Ulikuwa usiku mgumu sana," alisema
Wenger. "Dortmund walikuwa timu bora. Tulikuwa na kiwango kibovu.Ni
vigumu kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja kwasababu kama timu hatujawa
katika kiwango sawa"
"Tatizo liko pale pale, tulipata nafasi
za kufunga kipindi cha kwanza. Tulikamatwa katika mashambulizi mawili ya
kushitukiza. Kwa mara ya kwanza tulipoteza mpira mita 80 kutoka kwenye
goli letu. Kulikuwa na watu wengi wa kuzuia goli hilo. Bado tulikuwa
watu watatu dhidi ya mmoja. Ni ngumu kuelewa jinsi gani tulifungwa"
0 maoni:
Post a Comment