Tuesday, June 9, 2015


Liverpool wameafikiana dili ya kunsaini Kijana wa Miaka 22 anaecheza kama Straika wa Burnley iliyoporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu England licha ya Klabu hiyo kuigomea ofa ya Liverpool.
Danny Ings, anaechezea Timu ya Taifa ya England ya U-21, anamaliza Mkataba wake na Burnley mwishoni mwa Mwezi huu lakini kutokana na umri wake mdogo Kanuni zinaitaka Liverpool kuilipa fidia Burnley.
Liverpool wanatarajia kulipa fidia ya kati ya Pauni Milioni 5 hadi 6 lakini ikiwa Burnley watagoma basi suala hilo litaenda kwenye Jopo litakaloamua idadi inayofaa.
Wakati Burnley imesema itaendelea maongezi na Liverpool, Vigogo hao wa England wametangaza watamsaini Ings Julai 1 baada ya kukubaliana malupulupu yake binafsi na ikiwa Mchezaji huyo atafuzu upimwaji afya yake.

Msimu uliopita, ukiwa ni Msimu wakevwa kwanza kucheza Ligi Kuu England, Ings alipiga Bao 11 katika Mechi 35 alizoichezea Burnley wakati Mastraika wanaotambulika huko Liverpool, Daniel Sturridge, Rickie Lambert, Mario Balotelli na Fabio Borini, wakifunga jumla ya Bao 8 tu huku Raheem Sterling akipiga 7 na Steven Gerrard kufunga 9.
Ings atakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Liverpool wakati huu baada ya Wiki iliyopita kumpata Mchezaji Huru kutoka Man City James Milner.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog