Friday, September 18, 2015


KASEJA...

Kipa Juma Kaseja, kesho anatarajia kuweka rekodi iwapo ataichezea Mbeya City.


Mbeya City inatarajia kuchuka dimbani kwa “Mbeya derby” dhidi ya wapinzani wao wakubwa Prisons.

Mechi hiyo inachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kama Kaseja atakuwa langoni, atakuwa kwa mara nyingine anajumuika kwenye mechi ya watani nje ya Dar es Salaam.

Kaseja ni kati ya wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi za watani lakini ni akiwa Simba mara nyingi zaidi na akiwa Yanga pia wakati wakiivaa Simba.

Lakini safari hii, Kaseja anacheza derby ambayo itakuwa haihusishi timu za Dar es Salaam au timu kongwe za Yanga na Simba.


Kocha Juma Mwambusi amesema ana imani na kiwango cha Kaseja na akiamka salama, yuko tayari kumtumia hiyo kesho.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog