Friday, September 18, 2015



Beki wa Tanzania Prisons, James Josephat ameendeleza rekodi ya timu yake ya kutoa mchezaji wa kwanza kupata kadi nyekundu katika Ligi Kuu Bara.

Beki huyo alipata kadi hiyo juzi baada ya kumfanyia madhambi kiungo wa Yanga, Simon Msuva na kupewa kadi nyekundu akiwa ndiyo wa kwanza msimu huu. Ilikuwa ni katika mchezo wao dhidi ya Yanga ambao walifungwa mabao 3-0.
Msimu uliopita wa 2014/15, Prisons ndiyo walitoa mchezaji wa kwanza kupata kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Yanga ambao walifungwa mabao 2-1.
Timu hizo zilikutana Septemba 28, 2014 katika mchezo wa pili wa ligi hiyo ambapo beki wa Prisons, Jacob Mwaitalako alilimwa kadi nyekundu akiwa mchezaji wa kwanza kupata kadi hiyo katika msimu huo.

Hivyo, Prisons imeweka rekodi kwa wachezaji wake kwa msimu miwili kufungulia kwa kadi nyekundu, lakini pia michezo yote hiyo ni dhidi ya Yanga.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog