Kijana mpya: Loic Remy ameamua kuchukua jezi namba 18 baada ya kujiunga na Chelsea jumapili iliyopita.
MSIMU ujao, Loic Remy hatavaa jezi namba 9 inayosemekana kuwa na gundu katika klabu ya Chelsea.
Kuondoka kwa Fernando Torres kumeifanya jezi hiyo ambayo kwa utamaduni anavaa mshambuliaji wa kati ibaki bila mtu.
Lakini Remy ambaye amejiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 10.5 akitokea Queens
Park Rangers, amechagua kuvaa jezi namba 18 na ilithibitishwa jana
usiku wakati klabu hiyo ya ligi kuu ikitangaza orodha ya wachezaji 25 wa
timu hiyo sambamba na namba za jezi zao.
Jezi namba 9 itabaki bila mtu mpaka mwezi januari na hii inawezekana ikawa moja ya historia nzuri ya karibuni.
Gundu? Wachezaji wa Chelsea wameonekana kuiogopa jezi namba 9 aliyokuwa anavaa Ferando Torres.
Mabadiliko: Didier Drogba aliomba jezi namba 11 kwa Oscar baada ya awali kupewa jezi namba 15
Torres alifunga mabao 20 katika mechi za ligi kuu kwa miaka mitatu na nusu aliyokaa Stamford Bridge.
Mchezaji aliyemtangulia kuvaa jezi hiyo Franco
Di Santo,alishindwa kufunga bao lolote na Steve Sidwell na Khalid
Boulahrouz hawakufurahia maisha yao Chelsea wakivalia jezi hiyo.
Kabla ya hapo, mshambuliaji wa Argentina, Hernan Crespo, katika msimu wake mmoja akivalia jezi hiyo alifunga mabao 10 tu.
Mateja Kezman aliwasili Chelsea
akitokea PSG alikofunga mabao 78 katika misimu miwili nchini Uholanzi,
lakini akivalia jezi namba 9 katika klabu ya Chelsea alifunga mabao 7
tu.
Petr Cech ameendelea kuvalia jezi namba 1 licha ya Thibaut Courtois kuanza msimu huu kama kipa chaguo namba moja kwa kocha Jose Mourinho.
0 maoni:
Post a Comment