Monday, July 28, 2014

Liverpool imemsaini Beki wa Southampton Dejan Lovren kwa Dili inayoaminika ni Pauni Milioni 20 na huyo ni Mchezaji wao wa 5 kumnunua kwa ajili ya Msimu mpya.
Lovren, mwenye Miaka 25, ni Sentahafu kutoka Croatia na amesaini Mkataba wa Miaka Minne.
Lovren anaungana na Wachezaji wengine wawili waliotoka Southampton na kuhamia Liverpool katika kipindi hiki ambao ni Rickie Lambert na Adam Lallana.

Meneja Brendan Rodgers amesema usajili huu wa Mchezaji huyo ni muhimu mno kwao na Lovren atasafiri moja kwa moja kwenda Marekani kujiunga na Liverpool ambayo inashiriki Mashindano ya International Champions Cup.
Lovren alijiunga na Southampton kutoka Lyon Mwaka Jana kwa Dau la Pauni Milioni 8.5 na anaondoka Klabu hiyo akiwa amebakisha Miaka Mitatu kwenye Mkataba wake.

Hadi sasa Southampton, kwenye Kipindi hiki cha Uhamisho, imeshawauza Wachezaji Watano kwa Jumla ya Pauni Milioni 92.Wachezaji wengine walioondoka Klabu hiyo ni Luke Shaw aliekwenda Man United, Calum Chambers anaekwenda Arsenal, na wawili waliohamia Liverpool, Rickie Lambert na Adam Lallana.


Dejan Loven amesaini kwenda Liverpool kwa pauni £20m kutoka  Southampton

 Lovren sasa ni Beki wao mpya na hatari

Lovren anatarajiwa kujiunga na Wachezaji wa Liverpool kwenye Ziara kujiandaa na Msimu mpya wa 2014/15 unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Watano walionunuliwa na Liverpool:
-Straika: Rickie Lambert, Miaka 32, Pauni Milioni 4 kutoka Southampton
-Kiungo: Adam Lallana, Miaka 25, Pauni Milioni 25 kutoka Southampton
-Kiungo: Emre Can, Miaka 20, Pauni Milioni10 kutoka Bayer Leverkusen
-Winga: Lazar Markovic, Miaka 20, Pauni Milioni 20 kutoka Benfica
-Beki: Dejan Lovren, Miaka 25, Pauni Milioni 20 kutoka Southampton

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog