Tuesday, July 29, 2014

Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama leo alifuturisha wasanii, ndugu,jamaa na marafiki zake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka marehemu mama yake mzazi ambaye alishatangulia mbele ya haki. Akitoa shukrani zake kwa waalikwa, alisema ameona vyema kuandaa chakula cha pamoja ili waweze kumuenzi mama yao mzazi kwa vile alipenda sana watu hasa kukutana na kupata chakula pamoja.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiendelea kutoa shukrani zake za pekee.

Mjomba wa Msanii chipukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akitoa shukrani zake za pekee.

Msanii wa runinga, Michael Deodatus Sango ‘Mike’ akitoa shukrani kwa niaba ya rais wa Bongo Movie Steve Nyerere ambaye hakuweza kufika.
Wasanii, ndugu jamaa na marafiki waliofika wakipata futari.
Kila mmoja hakuwa nyuma kupata futari.
Huduma zikiendelea kutolewa.
Kumbu Kumbu.
Picha ya pamoja na wasanii wenzake mara baada ya kupata futari.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama (kati) akiwa na Dada yake kushoto na mdogo wake wakipata ukodak.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiwa na wajomba zake.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog