Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (kulia),
akimakabidhi Bendera ya Taifa, mmoja wa wachezaji wa timu ya Taifa wa
mchezo wa Chess, Hemed Mlawa (wa pili kushoto), Dar es Salaam leo
asubuhi kwa ajili ya kuondoka kesho kwenda kushiriki mashindano ya
kimataifa nchini Norway. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya
Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini,
kushoto ni mchezaji Emmanuel Mwaisumbe. Safari hiyo imedhaminiwa na
Tanzania Chess Foundation na Kasparov Foundation.
Hapa ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati), Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini
(kulia), mchezaji Hemed Mlawa (kushoto) na Emmanuel Mwaisumbe (wa pili
kushoto), wakifurahi baada ya kucheza mchezo huo wakati wakiwaonesha
waandishi wa habari.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati),
akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa
mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo
hapa nchini, akizungumza na wanahabari. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo hapa nchini, akizungumza na wanahabari.
Wachezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa (kulia) na Emmanuel Mwaisumbe
wakiwa kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa bendera ya Taifa. Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania, Henry Lihaya.
Kulia ni Mratibu wa Chess Tanzania, Johnson Mshana akifuatilia kwa karibu tukio hilo. Kushoto ni Mwanahabari
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi (katikati),
akizungumza na wanahabri kabla ya kukabidhi bendera. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa
mchezo huo hapa nchini na kulia mchezaji Hemed Mlawa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Spicenet, Vinay Choundry ambaye ni muasisi wa mchezo huo
hapa nchini na mchezaji wa mchezo huo, Hemed Mlawa wakionesha umahiri wa
kucheza mchezo huo mbele ya wanahabari.Katikati ni Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Dioniz Malinzi na mchezaji
Emmanuel Mwaisumbe. (Imeandaliwa na www.habari za jamii.com- simu namba
0712-727062, 0786-858550)
…………………………………………………………………………………………..
Dotto Mwaibale
TIMU
ya Taifa ya Chess imeagwa Dar es Salaam leo asubuhi kwajili ya kwenda
kushiriki mashindano ya chess 41 ya kimataifa Olympiads yatakayofanyika
nchini Norway.
Jumla ya wachezaji watano wataondoka nchini leo usiku kwenda kushiriki mashindano hayo.
Wachezaji hao ni Geofrey Mwanyika, Hemed Mlawa, Emmanuel Mwaisumbe, Nurdin Hassuji na Yusuph Mdoe.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi timu hiyo bendera ya taifa, Mwenyekiti wa
Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi alisema kuwa kuwakabidhi
bendera hiyo ni ishara ya kuwatakia safari njema na ushindi katika
mashindano hayo.
Malinzi
alisema anashukuru wale wote ambao wamekuwa katika mstari wa mbele
kusimamia mchezo huo nchini hadi kufikia kushiriki mashindano ya
kimataifa.
”Namshukuru
sana Mr Vinay kwa msaada wake anaoutoa kusapoti mchezo huu Tanzania na
kwa moyo wake wa kutoa, maana waswahili husema kutoa ni moyo na sio
utajiri maana kuna matajiri wegi lakini sio watoaji” alisema
Aliongeza kuwa anamatumaini kuwa wachezaji hao watakwenda kufanya vizuri katika mashindano hayo na kuitangza Tanzania.
Naye
Mkurugenzi wa Kampuni ya Spicenet na Mwanzilishi wa Mchezo wa Chess
Tanzania, Vinay Choudary alisema kwa yeyote atakayeweza kuibuka na
ubingwa shilingi milioni mia moja zitatolewa kwa ajili yake.
Choudary
alisema hadi sasa walipofikia ni pazuri kwa Tanzania kushiriki
mashindano ya kimataifa hivyo anawatakia safari njema na ushindi katika
mchezo huo.
Mchezaji Hemed Mlawa alisema wataiwakilisha vema Tanzania na watahakikisha wanafanya vizuri.
”Hii
ni mara ya kwanza sisi kushiriki hivyo hatuwezi kusema kuwa tutarudi na
ushindi moja kwa moja bali tutafanya vizuri na tunaamini tunaweza
kuzishinda baadhi ya nchi”alisema
Mashindano hayo ni ya wiki mbili na yameratibiwa na Shirikisho la Chess Duniani(FIDE)
na kudhaminiwa na Tanzania Chess Association na Kasparov Association.
0 maoni:
Post a Comment