JOSE
Mourinho amefurahishwa na urejeo wa Didier Drogba na anatarajia mshambuliaji
huyo ataisaidia Chelsea msimu uliopita.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alisaini mkataba wa mwaka mmoja ijumaa ya wiki
iliopita kufuatia mkataba wake kumalizika na klabu ya Galatasaray ya Uturiki.
Drogba
alifurahia miaka nane akiwa darajani, kuanzia mwaka 2004 hadi 2012.
Nyota
huyo mwenye miaka 36 alijiunga na kikosi cha Chelsea siku ya jumapi ambapo walishinda
mabao 2-1 dhidi ya Olimpiji katika mechi ya maandalizi ya kabla ya msimu,
lakini hakucheza.
“Awali
ya yote, alipokuja, ilionekana kama hajawahi kuondoka klabuni,” Mourinho aliwaambia waandishi wa habari. “Ilikuwa
kawaida sana, hakukuwa na jipya kwasababu anamjua kila mtu na kila mtu anamjua”.
“Siku
zote alikuwepo hapa hata kama hakuwepo hapa. Chelsea ni klabu yake, hata miaka miwili ambayo alikuwa mbali na
kuzichezea klabu za Galatasaray na Shanghai (Shenhua)”.
“Kwahiyo inaonekana kama alikwenda kwenye mapumziko mafupi na kurudi tena, kila kitu ni kawaida. Lakini kweli, nadhani tunamhitaji sana. Tunamtaka kaka mchezaji wa kikosi chetu ili kiwe kama ninavyotaka”.
0 maoni:
Post a Comment