Luis Suarez, alitia muhuri katika jezi na bendera ya Uruguay na kuwatupia mashabiki nje ya nyumba yake.
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 11:07 jioni
BARCELONA inatarajia kumpa majukumu mpya
nyota wake Lionel Messi ambapo sasa atacheza nyuma ya washambuliaji
wawili, Luis Suarez na Neymar, kwa mujibu wa ripoti za Hispania.
Kuelekea msimu ujao, Kocha Luis Enrique anataka kuwatumia washambuliaji wote watatu kwa wakati mmoja ndani ya kikosi chake.
Enrique anaamini kumhamisha Messi katika
nafasi aliyozoeleka kucheza na kumchezesha nyuma upande wa kulia,
kutawafanya Suarezi na Neymar wang`are zaidi.
Mabadiliko: Lionel Messi anatarajiwa
kupewa majukumu mapya katika klabu yake ya Barcelona, sasa atacheza
nyuma ya Suarez na Neymar.
Mtu muhimu: Neymar ataungana na Suarez
kuongoza safu ya ushambuliaji ya Barcelona baada ya kupona majeruhi yake
ya kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Suarez amefungiwa mpaka mwezi oktoba
mwaka huu kwa kitendo cha kumng`ata beki wa Italia , Giorgio Chiellini
kwenye mechi ya makundi ya kombe la dunia nchini Brazil.
Baada ya kitedo hicho aliamua kuondoka Liverpool na kujiunga na Barca kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75.
Wakatalunya wanasemekana kuanza harakati za kukata rufani juu ya adhabu hiyo.
Barcelona pia wanamsubiri Neymar apone majeruhi yake aliyoyapata kombe la dunia hatua ya robo fainali.
Taifa mwenyeji bila Neymar lilipigwa mabao 7-1 kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Wakati huo huo, Messi alitajwa kuwa
mchezaji bora wa mashindano licha ya Argentina kufungwa bao 1-0 dhidi ya
Ujerumani katika mechi ya kfainali.
0 maoni:
Post a Comment