Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 8:00 mchana
Viingilio
kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji itakayochezwa keshokutwa
(Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh.
30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu.
Kuanzia
kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za kielektroniki zitauzwa pia katika
magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry
Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya
Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa
Taifa.
Aidha
tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza
4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000
kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka
kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza 1 kukubali.
Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo
vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa
Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre,
Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions
(Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket
(City Centre, Kibo Tegeta na Upanga).
Vodashop
(Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol
Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach),
Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA
(Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa
Karume.
0 maoni:
Post a Comment