Wednesday, April 22, 2015


Sina mbavu mieee nipisheeee!!! Chicharito baada ya kuizima Atletico Madrid usiku huu!Chicharito akishangilia bao lake la pekee baada ya kuifungia na kuipa Ushindi Real usiku huu dhidi ya Atletico Madria kwenye marudiano ya Klabu Bingwa Ulaya. Bao hilo limewapeleka Real Madrid Nusu Fainali ya 31 na Droo ya Nusu Fainali itachezeshwa Ijumaa ya wiki hii.Javier Hernández aliwafungia bao Real Madrid dakika za majeruhi na kufanya 1-0 dhidi ya Atletico Madrid, Ni Baada ya kupewa pasi ndani ya boksi na Staa wa Real Cristiano Ronaldo na kufunga bao hilo la Ushindi. Real wamesonga hatua ya Nusu faonali kwa Ushindi wa bao la Chicharito. Mtanange huu pia Atletico Madrid walimaliza pungufu wachezaji 10 Uwanjani baada ya mwenzao Arda Turan kuoneshwa kadi njano ya pili na kuoneshwa kadi Nyekundu kwa kumchrzea rafu mbaya mchezaji wa Real Madrid Sergio Ramos.Cristiano Ronaldo akiendesha..mpira wakati wa kipindi cha kwanza
Chicharito hoi! akishangaa kuona mpaka kipindi cha kwanza kinakatika bado 0-0, Ngoma ngumu!Ronaldo akiachia shutiRonaldo tena..Arda Turan akioneshwa kadi ya njanoSergio Ramos kwenye patashika mpira wa kichwa!Arda Turan akimwangaisha Fabio wa RealRonaldo akijishika kichwa katika kipindi cha kwanzaSergio Ramos chini akijiuguza katika kipindi cha kwanza.Kikosi cha Real Madrid kilichoanza dhidi ya Atletico MadridKikosi cha Atletico MadridDiego Semeone na Carlo Ancelotti wakisaliniana kabla ya kipute kuanza BernabeuMashabiki wa Real madrid wakiwapungia Mastaa waoVIKOSI:
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Coentrao, Pepe, Kroos, Isco, Rodriguez, Ronaldo, Hernandez.
Akiba: Navas, Arbeloa, Khedira, Lucas Silva, Illarmendi, Jese.
Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Miranda, Godin, Jesus Gamez, Tiago, Koke, Saul, Arda, Griezmann, Mandzukic.
Akiba: Moya, Siqueira, Gimenez, Raul Garcia, Gabi, Jimenez, Torres.
Refa: Felix Brych
Robo Fainali-Mechi za Marudiano
Mechi zote mbili kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku

Jumatano Aprili 22
Real Madrid vs Atletico Madrid [Santiago Bernabeu, Madrid, Spain] [0-0]
AS Monaco vs Juventus [Stade Louis II, Monaco, France] [0-1]

Wachezaji wa Atletico Madrid Joao Miranda, Antoine Griezmann na Mario Mandzukic wakipasha kwenye Uwanja wa Bernabeu usiku huu, Tayari kwa marudiano ya Robo Fainal, Mshindi kwenda Nusu Fainali

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog