Thursday, August 28, 2014



IMG_6809.JPG

Wiki kadhaa baada ya kuteuliwa kuwa nahodha mpya wa Manchester United, mshambuliaji Wayne Rooney leo amepata uongozi mpya kwenye medani za soka.
Rooney ameteuliwa na kocha Roy Hodgson amemteua mshambuliaji huyo kuwa nahodha mpya wa timu hiyo ya taifa.
Rooney mwenye miaka 28 amechukua mikoba iliyoachwa na kiungo wa Liverpool, Steven Gerrard aliyestaafu.
Rooney aliwahi kuvaa kitambaa cha unahodha akiiongoza England kwenye mechi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya San Marino, Oktoba 2012.

Staa huyo amewapiku wachezaji wenzake kipa Joe Hart na beki Gary Cahill ambao nao walikuwa wakitajwa kuchukua uongozi huo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog