Malkia Elizabeth ameifungua
rasmi michezo hiyo kwa kuusoma ujumbe wake uliokuwa umehifadhiwa katika
kile kinachofahamika kama the Commonwealth baton yaani mwenge wa jumuiya
ya madola.
Maelfu ya wanamichezo kutoka nchi 71 wameshiriki
katika ufunguzi huo mbele ya watu elfu 40 waliokuwa uwanjani huku dunia
ikifuatilia kupitia vyombo vya habari.Hali ya hewa katika mji wa Glasgow leo imetambulishwa rasmi kuwa ndiyo yenye joto Zaidi kwa mwaka huu baada ya kufikia digrii 25c.
Michezo hiyo itahusisha michezo 17 kwa siku 11.
Michezo ya jumuiya ya madola uhusisha nchi zilizowahi kuwa chini ya utawala wa himaya ya uingereza.
0 maoni:
Post a Comment