Thursday, July 24, 2014

IMG_0618 
Kikosi cha Mtibwa Sugar msimu uliopita. Mlinda mlango Hussein Sharrif `Casillas` amejiunga na Simba majira haya ya kiangazi na kusaini mkataba wa miaka miwili
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU nyingi zinazoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara zipo katika maandalizi ya kujiwinda na msimu mpya utakaoanza kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Wakata miwa wa mashamba wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wapo jijini Dar es salaam kujifua katika fukwe za Koko ili kujiimarisha zaidi.
Mtibwa Sugar chini ya kocha mkuu, Mtanzania Mecky Mexime, msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 7 kwa kujikusanyia pointi 31 kibindoni.
Mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000 walishinda mechi 7, sare 10 na kufungwa mechi 9. Walitikisa nyavu za wapinzani mara 30 na zao kuguswa mara 31.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog