MECHI
kati ya timu Israeli ya Maccabi dhidi ya Lille ya Ufaransa iliahirishwa
baada ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina kuvamiwa uwanja.
Waandamanaji
hao walioripotiwa kuwa na asili ya Uturuki waliingia katika uwanja wa
Austrian ambapo mchezo ulikuwa unaendelea na kuwavamia wachezaji wa
Maccabi na kuzua vurugu.
Mmoja wa wachezaji alionekana akizozana na shabiki kabla ya kuanza kurushiana makonde mazito.
Hata hivyo wachezaji wa Maccabi walifanikiwa kutoka uwanjani bila kujeruhiwa.
Tukio hili limekuja wakati huu ambao majeshi ya Israel yamevamia na kufanya uhalifu dhidi ya majeshi ya Hamas huko Gaza.
Mashambulizi: Waandamanaji walivamia uwanja na kuanzisha dhoruba ya kuwashambulia wachezaji wa Maccabi Haifa
Hatari sana: Waandamanaji waliwavamiwa wachezaji wa Maccabi Haifa na kusababisha mechi kuahirishwa.
0 maoni:
Post a Comment