Raha tupu: Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney akimpongeza Danny Welbeck baada ya kufunga bao la kwanza.
LOUIS Van Gaal ni kiboko. Awaonya Jose Mourinho na Asernal Wenger kuwa amekuja kufanya kazi Old Trafford.
Jana usiku ameshusha majanga kwa
LA Galaxy baada ya kuitandika mabao 7-0 katika mchezo wa kirafiki wa
maandalizi ya kabla ya Msimu nchini Marekani.
Hii imezidi sasa! Van Gaal
atakuwa anawaomba viongozi wa Manchester United kuipeleka timu kwenye
ziara ya maandalizi ya kabla ya msimu kila majira ya kiangazi.
Ikiwa ni siku moja tu imepita
tangu alalamike kuhusu ziara ya Marekani kwa madai kuwa inawafanya
wachezaji wake wachoke, kocha huyo mpya wa Man United aliitazama timu
yake ikipata ushindi mkubwa na kuonesha kiwango kizuri.
Mwanzo mzuri: Welbeck akishangilia baada ya kuifungia Man United goli la kuongoza katika dakika ya
0 maoni:
Post a Comment