Thursday, July 24, 2014




Akizungumza na Mwanaspoti, Coutinho raia wa Brazil alisema kwa sasa bado hawezi kusema moja kwa moja kuwa ana uhakika wa kuingia katika kikosi cha kwanza cha Yanga kwa vile hajajua uwezo wa wenzake wanaocheza nafasi kama yake ambao wapo katika vikosi vya mataifa yao. 

KIUNGO wa Yanga, Mbrazil Andrey Coutinho (pichani )amesema anafurahia zaidi staili ya uchezaji ya kiungo Nizar Khalfan na kwamba ndiye kiungo anayejua zaidi wapi kwa kumwekea mpira anapokuwa akikimbia.

Coutinho aliliambia Mwanaspoti kuwa, “ Yanga ina viungo wengi na wote wazuri lakini nimependa jinsi Nizar anavyocheza kwani anaonekana kujua jinsi mimi ninavyotaka kupewa pasi nikiwa nakimbia.

“Kwanza naona ana nguvu lakini pili anapiga pasi kwa kukuwekea pale ulipo, napenda hata kwenye mazoezi niwe napangwa naye kwani ananifanya nicheze kwa ufasaha zaidi na kufanya malengo yangu kutimia vizuri.

“ Pia ana uwezo mzuri wa kupiga pasi pia kupiga mashuti ya nguvu ambayo yanaweza kuwa na faida pale kipa anapotema na straika wetu akanasa mpira,” alisema.

Katika hatua nyingine kiungo huyo amesema  kuwa bado hajawa mpenzi wa vyakula vya Kitanzania kwa kuwa hapendezwi sana na ulaji wa vyakula vingi vya Kitanzania vya asili.
“Vyakula vya asili sijavizoea, nimevizoea vya kwetu kule Brazil, huku Tanzania napenda zaidi kula kuku, nyama ya kusaga ‘Beef’ na tambi pamoja na wali kwani ndiyo vyakula ambavyo utakavyoweza kuvikuta kwetu Brazil,” alisema

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog