Tuesday, October 13, 2015


Mchezaji wa Manchester United Memphis Depay amekwaruzana na Mchezaji wa zamani wa Klabu hiyo Robin van Persie wakati wa mazoezi wa Timu ya Taifa ya Netherlands. Tukio hilo limethibitishwa na Kocha wa Netherlands Danny Blind lakini amepuuza umuhimu wake na imefahamika kuwa lilitokea kabla ya Mechi ya Jumamosi ya EURO 2016 ambayo Netherlands iliifunga Kazakhstan 2-1.
Kocha Blind, ambae mwanawe, Daley, ni Mchezaji mwenzake Depay huko Man United ambae pia yumo Timu ya Taifa ya Netherlands, alieleza: “Yapo matukio mazoezini ambapo Wachezaji hutofautiana. Mnayazungumza. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa na yamekwisha.”
Blind pia alisisitiza kuwa tukio hilo halikumfanya ampige Benchi Van Persie kwenye Mechi na Kazakhstan ambayo aliingizwa Kipindi cha Pili na kufikisha Mechi 100 kwa Nchi yake.
Pia Van Persie, ambae aliihama Man United Mwezi Julai kwenda Fenerbahce ya Uturuki ukiwa ni Mwezi mmoja tu baada ya Depay kuhamia Man United, ndie Mfungaji Bora wa Holland katika Historia ya Nchi hiyo akiwa na Bao 49.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog