Thursday, August 13, 2015


David De Gea hatarudi kwenye Kikosi cha Manchester United dhidi ya Aston Villa hapo Ijumaa huko Villa Park kwa mujibu wa Meneja Louis Van Gaal.
Kipa wa Kimataifa wa Argentina Sergio Romero ataendelea kuwa Golini kama alivyofanya Jumamosi iliyopita huko Old Trafford Man United ilipoifunga Tottenham 1-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya wa 2015/16.
Hivi sasa Kipa David De Gea yupo kwenye sakata kubwa la kutaka kuhamia Real Madrid huku Man United ikitia ngumu na kutaka kitita kikubwa.
Kwenye Mahojiano hayo ya Leo yaliyofanyika huko Carrington kwenye Kituo cha Mazoezi cha Man United kuzungumzia Mechi yao ya pili ya Ligi hapo Kesho, Van Gaal alisema msisitizo wao mkubwa ni kushinda Mechi za Ugenini tofauti na Msimu uliopita ambao ulikuwa Msimu wake wa kwanza tu ambapo walishinda Mechi 6 tu.
Van Gaal ameeleza kuwa Msimu uliopita wao walikuwa bora Nyumbani Old Trafford na rekodi hiyo iliwafanya wawe wa 3 katika Timu zilizofanya vizuri Nyumbani kwenye Ligi.
Meneja huyo pia alihojiwa kuhusu matamshi ya Straika wa zamani wa Barcelona Hristo Stoichkov ambae amemtaka Pedro kutohamia Man United kwa sababu yake yeye Van Gaal.
Stoichkov, aliecheza chini ya Van Gaal katika Miaka ya 1990 huko Barca, amedai Van Gaal huzibomoa Klabu kwa sababu ya uduni wake.

Van Gaal alijibu: “Siku zote humtazama nani kasema maneno na kisha najua kwa nini. Hainisumbia. Yeye ndie alikuwa Mchezaji wa kwanza kumtosa [kumuuza] na ndio maana anasema hivyo.”
Huku Manchester City na Chelsea wakipambana huko Etihad hapo Jumapili, Waandishi walidokeza kuwa ushindi kwa Man United Ijumaa huko Villa Park utawafanya wachepuke haraka mbele ya Vigogo hao lakini Van Gaal alisema: “Ushindi utatupa mwanzo mzuri kupita Msimu uliopita. Lakini ni mapema na Msimu ni mrefu.”
Kuhusu Javier Hernandez ‘Chicharito’, Van Gaal alieleza: “Straika ni Rooney na Chicharito ni Straika wa Pili na yeye anajua hilo.”
Alipoulizwa kuhusu habari kuwa Adnan Januzaj anauzwa, Van Gaal: “Hauzwi.”

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog