Thursday, April 16, 2015


Yanga, Wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia kwenye michuano ya Klabu Barani Afrika, Jumamosi wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Etoile du Sahel ya Tunisia katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho.Yanga imetua hatua hii baada ya kuzibwaga BDF XI ya Botswana na FC Platinum ya Zimbabwe katika Raundi za awali.
Akizungumzia Mechi hii, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema ni muhimu kushinda Mechi hii ya Nyumbani na pia kuwa makini na staili ya kupoteza muda ambayo Etoile du Sahel wanategemewa kuitumia.Yanga inatarajiwa kuwatumia tena Wachezaji wao muhimu ambao walikuwa Majeruhi ambao ni Salum Telela na Coutinho.
Etoile du Sahel inatarajiwa kutua Dar es Salaam leo hii kwa Ndege ya kukodi.

CAF KOMBE LA SHIRIKSHO
Mechi za Kwanza Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi kuchezwa Wikiendi ya Aprili 18

Association Sportive Olympique de Chlef vs Club Africain
Djoliba AC vs Hearts of Oak
Young Africans vs E.S. Sahel
Royal Leopards vs AS Vita Club
Onze Createurs vs ASEC Mimosas Abidjan
Warri Wolves vs Etanchéité
CF Mounana vs Orlando Pirates
Al Zamalek vs Fath Union Sport de Rabat

Marudiano Wikiendi ya Mei 5

Washindi 8 wa Raundi hii watajumuika na Timu 8 zilizobwagwa nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na kuwekwa kwenye Droo maalum kupanga Mechi 8 za Mtoano na Washindi wake 8 kutinga hatua ya Makundi ambayo yatakuwa na Makundi mawili ya Timu 4 kila mmoja yatakayocheza Mtindo wa Ligi wa Nyumbani na Ugenini.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog