Star wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) ambaye kwasasa anatamba na filamu mpya ya Bad Luck kutoka Rj Company amewashukia baadhi ya ma-producer wa filamu nchini kwa kubagua baadhi ya wasanii wa kucheza filamu zao kwa kudhani kuwa ndiyo tiketi ya kuwapoteza kwenye tasnia hiyo. Kupitia twitter batuli aliandika "morning kwenu producers mnaohisi usipomshirikisha msanii fulani kwenye kazi zako za filamu ndiyo utampoteza kwenye fani kalagabaho#Mungu yupo"
Batuli hakuishia hapo bali aliendelea kutoa dozi kwa baadhi ya waigizaji wenzake wenye tabia za kupeleka maneno ya kinafiki na kuwawekea mastaa wenzao kauzibe kwa wasambazaji wa filamu ili wasinunue kazi zao "morning kwenu mastar mnaomaliza mafuta na pumzi zenu kwenda kuweka giza kwa wasambazaji wa filamu wasinunue kazi za ma-star wenzenu#jiamini" ali-tweet Batuli
kama wewe ni shabiki wa star huyo basi like page yake facebook BATULI ACTRESS m-follow hapa katika twitter BATULI ACTRESS
0 maoni:
Post a Comment