Tuesday, December 8, 2015


Mechi pekee ya Ligi Kuu England huko Goodison Park, Merseyside, Jijini Liverpool, Wenyeji Everton walijinasua toka kwenye kipigo na kutoka Sare ya 1-1 na Crystal Palace.
Bao za Mechi hii zilifungwa na Scott Dann Dakika ya 76 kwa Palace na Romelu Lukaku kurudisha Dakika ya 81.

Kabla ya Lukaku, mwenye Miaka 22, kusawazisha, Everton walipiga Posti mara 3 na hatimaye Lukaku kufunga likiwa ni Bao lake la 50 katika Mechi 100 za Everton.
Matokeo haya yamewaweka Palace Nafasi ya 6, wakiwa na Pointi 23, na Everton wakiwa Nafasi ya 9 wakiwa na Pointi 22 huku Vinara ni Leicester City wenye Pointi 32 baada ya Mechi 15 kwa Timu zote.
Scott Dann akishangilia bao lake Scott Dann akitupia kwa kichwaJason akiendesha mpira huku akinyemelewa na mchezaji wa Everton BrendanYohan Cabaye akituliza kwa uzuri
Meneja wa Everton Martinez Everton v Crystal Palace
Meneja wa Crystal Palace Alan PardewWayne Rooney nae alikuwepo na Mtoto wake KaiArouna akipenya!

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog