Thursday, June 4, 2015


www.bukobasports.comShirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
Ifuatayo ni hotuba ya Rais wa TFF , Jamal Malinzi aliyoisoma wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za timu za Taifa, uzinduzi wa tovuti mpya ya TFF na kutunuku vyeti kwa viongozi mbalimbali, makocha, wachezaji na wadhamini.
Mh Said Mtanda Mbunge wa Jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii
Mzee Said el Maamry Mwenyekiti Msataafu wa FAT
Ndugu Leodeger Tenga Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF na Rais mstaafu wa TFF
Ndugu wageni waalikwa
Ndugu waandishi wa habari
Mabibi na mabwana
Salam aleikum.

Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutufikisha hapa leo na kwa mafanikio mbali mbali ambayo tumekuwa tukiyapata.Ninakushukuru sana ndugu mgeni rasmi kwa kuacha shughuli zako kuja kujiunga nasi asubuhi hii katika shughuli hii.
Ndugu mgeni rasmi,tarehe 08 oktoba 1964 Tanzania ilipata uanachama rasmi wa shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA. TFF tuliona jambo zito kama hili hatuwezi kuliacha lipite hivi hivi.Hivyo mwaka jana tuliamua kuenzi maadhimisho ya miaka 50 ya kujiunga na FIFA kwa kufanya mambo mambo matatu makubwa.
La kwanza ni kutoa vyeti maalum kwa watu binafsi na taasisi mbali mbali kwa kutambua mchango wao uliotukuka katika kuendeleza mpira wa miguu Tanzania.

Leo hii ndugu mgeni rasmi tutakuomba ukabidhi vyeti hivi kwa wawakilishi wa makundi kadhaa kwa niaba ya wenzao.Makundi haya ni pamoja na viongozi wa kitaifa wastaafu,mawaziri wa michezo wastaafu,viongozi waliopita wa TFF?
FAT,wakurugenzi wa idara ya michezo,wenyeviti na makatibu wa baraza la michezo la taifa,Timuya Taifa iliyocheza fainali za Afrika mwaka 1980,waamuzi,makocha,wachezaji wa timu ya Taifa na watangazaji mahiri wa michezo.Jumla tumetunuku vyeti 194.
Kiuhalisia idadi hii ni ndogo sana ukilinganisha na wingi na uzito wa michango ya wadau mbali mbali wa mpira katika miaka 50 iliyopita.
Tunaomba Watanzania wenzetu watuelewe katika hili kuwa hawa tutakaowatunuku vyeti hivi ni wawakalilisha wa wadau wote wa mpira Tanzania.
Ninaomba tusimame kwa muda mfupi tuwaombe ewadau wenzetu na viongozi wa mpira wa miguu ambao wako katika orodha hii na wametangulia mbele ya haki.
Ndugu mgeni rasmi katika kuenzi miaka 50 ya Tanzania kujiunga na FIFA leo hii pia tutatoa mchango wa fedha kwa makundi yenye mahitaji katika jamii.
Pesa hizi zinatokana na makusanyo mbali mbali ikiwemo makusanyo ya mechi ya ngao ya hisani ifanyikayo kila mwaka. Makundi haya ni pamoja na walemavu wa viuongo,walemavu wa ngozi na wasioona.
Kitendo hii ni moja ya juhudi za TFF kurudisha katika jamii kile tunachokusanya. Kila kundi litapewa shilingi milioni tano na tunaendelea kupokea maombi toka makundi mbali ya kijamii na tukiyapitisha tutaendelea kugawa fedha hizi.
Jambo la tatu tutakalolifanya leo litakuwa ni kuzindua rasmi tovuti mpya ya TFF (www.tff.or.tz). Tumeamua kufanya jamabo hili katika kuenzi miaka hamsini ya kujiunga na FIFA ili kutoa msisitizo kuwa sasa TFF na sisi tunajiunga Na kuendeleza mpira kisasa kulingana na teknolojia iliyopo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog