BEKI
wa Paris Saint-Germain, David Luiz amewaomba radhi Chelsea baada ya
kushangilia bao alilofunga ambalo lilisaidia kuing’oa timu yake hiyo ya
zamani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Luiz alifunga bao la
kusawazisha katika dakika ya 86 ya mchezo huo na kusababisha mchezo huo
kwenda katika muda wa nyongeza. Nyota
huyo wa kimataifa wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 amesema anaomba
radhi kwa kuonyesha hisia zake kwani ilikuwa vigumu kujizuia kutokana na
furaha aliyokuwa nayo. PSG
ilisonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kwa faida
ya bao la ugenini baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo huo.
Luiz amewahi kuichezea Chelsea mechi 143 katika mashindano yote na
kufunga mabao 12 kabla ya kuhamia PSG kwa kitita cha paundi milioni 40
Juni mwaka jana.
0 maoni:
Post a Comment