Friday, March 13, 2015



MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alex Oxlade-Chemberlain atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nne kutokana na majeruhi ya msuli wa paja. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 alipata majeruhi hayo katika mchezo wa Kombe la FA Jumatatu iliyopita ambao Arsenal iliifunga Manchester United kwa mabao 2-1. Sasa Chamberlain anatarajiwa kukosa mechi za Ligi Kuu kati ya timu yake dhidi ya West Ham United, Newcastle United na Liverpool pamoja na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Monaco wiki ijayo. Wenger amesema ni vigumu kutabiri muda gani haswa Chamberlain atakaa nje lakini anadhani itakuwa ni kati ya wiki tatu hadi nne. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa litakuwa jambo la kuhuzunisha kwa mchezaji huyo lakini msimu huu amecheza mechi nyingi na kuonyesha umuhimu wake.
Soma Zaidi Hapa »

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog