Wednesday, April 8, 2015


Aslay Isihaka maarufu kwa jina la ‘Dogo Aslay’ na  Bakari Abdul katuti ‘Beka’ wakiimba Moja ya Wimbo wao kwenye Ukumbi wa "Rest House" ukumbi wa Jeshi  Wilayani Biharamulo Mkoa wa Kagera kwenye Shoo yao iliyoweza kushuhudiwa na Mashabiki  wengi wa Muziki huo wa Bongo Flava katika Ukumbi huo Biharamulo. Shoo hiyo ilifanyika Usiku wa tarehe 07.04.2015 katika Siku maalum ya Hitma ya kumkumbuka Hayati, Muasisi wa Mapinduzi Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume ambayo ilipewa jina la "Karume Day".
Nyimbo kibao ikiwemo NITAJUTA, NISEME, WAMBEA, NITAKUPWELEPWETA ziliimbwa katika Ukumbi huo wa Rest House ambao ni Ukumbi wa Jeshi katika Mji huo.
Yamoto Band unakuwa umegusa majina ya Vijana Machachari wanne ambao ni Waimbaji wenye Sauti Tamu na Vipaji vya hali ya juu  kutoka Mikoa tofauti hapa Nchini Tanzania. Kundi hilo ambalo lilianza kuunguruma katika Mji wa Mwanza, Geita, Bukoba Mjini na pia kumalizia Burudani zake hapa Wilayani Biharamulo Mkoani Kagera na Vinaja hao kufanya vyema katika Miji hiyo.

Aslay na mwenzake wakiwajibika vilivyo jukwaani
Kundi hilo linaundwa na Aslay Isihaka maarufu kwa jina la ‘Dogo Aslay’, Mbwana Yusuph Kilungi ‘Maromboso’, Enock Deogratius ‘Enock Bella’ pamoja na Bakari Abdul katuti ‘Beka’.
Hakika ilikuwa Burudani
Nyomi ya kutosha usiku huo

‘Dogo Aslay’, Mbwana Yusuph Kilungi ‘Maromboso’ wakiwajibika Jukwaani

Maromboso akifanya yake kwa Mashabiki wao
Jerry kwenye picha akitokelezea na mashabiki
Kiongozi Mnec (kulia) Bw. Yusuph A. Khatry akiwa na Mama
Sunday(kulia) katikati ni Jonathan Mwanga --Waandaaji wa Shoo hiyo wakiwa na Rafiki yao kikazi Bw. Willy Kiroyera ambaye walikutana nae usiku huo wa shoo akitokea Nchi jirani ya Rwanda mjini Bujumbura kwenye shughuli za kitalii.


Wadau..wakifuatilia Muziki huo kwa makini..

Willy O. Rutta akipeana neno na Mtangazaji wa Radio Kasibante Fm Bw. Abdulrazak Majid(kulia) wakati wa Shoo hiyo ya Yamoto Band Biharamulo.



Wadau

Machote yote kwa Waimbaji wa Kundi la Yamoto Band.

Nani zaidi!!




Mashabiki wakiyarudi mangoma ya Live kutoka kwa Yamoto Band

Shabiki wa Yamoto Band nae akijinafasi mbele ya Mashabiki wenzake
Mambo ya Yamoto Band



Hatari sana! Burudani ikiendelea..
Bw. Jonathan Mwanga akipata ukodak na Shabiki wake Biharamulo usiku huu.

Dada moja wa waimbaji Chipukizi wa Said Fella Getrude akiwajibika jukwaani kwa kufokafoka Rap
Baadhi ya Mashabiki waliohudhuria katika shoo ya bendi ya YAMOTO  katika ukumbi wa Rest House jana usiku wakionekana kumkubali Dada huyo mkali wa Kurap .
Chiba akifanya yake huku akiwa kasimama kwa mguu mmoja  pekee
Kipaji ni kipaji

Waimbaji wanaounda kundi la “Yamoto Band”Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani sambamba na Kijana wao mwenye mguu mmoja Chiba"



0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog