Friday, October 9, 2015


Jurgen Klopp amekubali kuwa Meneja wa Liverpool kwa Mkataba wa Miaka Mitatu ambao anatarajiwa kuusaini Leo na Ijumaa kuanuliwa rasmi kama Meneja ,pya.
Klopp, Mjerumani mwenye Miaka 48, anamrithi Brendan Rodgers aliefukuzwa Jumapili iliyopita baada ya kudumu Miaka 3 ½ lakini Msimu huu Timu inasuasua na ipo Nafasi ya 10 kwenye Ligi Kuu England.
Klopp amekuwa hana kibarua tangu Mei alipoondoka Klabu ya Germany Borussia Dortmund baada ya kukaa nayo kwa Miaka 7.
Akiwa Liverpool, Klopp atakuwa nao Wasaidizi wake walewale aliokuwa nao Dortmund ambao ni Zeljko Buvac na Peter Krawietz.
Mechi ya kwanza ya Klopp akiwa na Liverpool, ambayo imeshinda Mechi 4 tu kati ya 11 iliyocheza Msimu huu, itakuwa ni ya Ligi Ugenini huko White Hart Lane Jijini London dhidi ya Tottenham hapo Oktoba 17.
Kwa sasa Ligi imesimama kupisha Mechi za Kimataifa na itarejea kilingeni hiyo hiyo Oktoba 17.

Klopp, ambae baada ya kustaafu uchezaji wake wa Soka akichezea Mainz ya Germany maisha yake yote ya Soka, alianzia kazi ya Umeneja akiwa hapo hapo Mainz na kisha kuhamia Borussia Dortmund.
Akiwa na Dortmund Klopp aliweza kutwaa Ubingwa wa Bundesliga mara 2, Mwaka 2011 na 2012, pamoja na DFB-Pokal Mwaka 2012, DFL-Supercup kwenye Miaka ya 2008, 2013 na 2014 na pia kuifikisha Klabu hiyo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2013.
Klopp amewahi kutwaa Tuzo ya Meneja Bora wa Germany mara mbili katika Miaka ya 2011 na 2012.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog