Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku mwanamuziki wa bendiya Vijana Jazz
Marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku aliyekuwa mwamuziki wa bendi ya Vjana Jazz enzi hizo.
…………………………………………………………………………………………
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku ni Mtoto wa mwanamuziki wa zamani marehemu Hemedi Maneti Ulaya Chiriku
aliyekuwa akiimba katika bendi ya umoja wa vijana Vijana Jazz enzi hizo
ambapo anasema amekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu japokuwa kama
ilikuwa kama kujifurahisha, Komweta Hemed Maneti alianza muziki kama
kazi mwezi Agosti mwaka 2013 akiimba katika bendi ya Vijana Jazz ambayo
marehemu baba yake Mzee Hemedi Maneti Ulaya aliitumikia kwa mafanikio enzi za uhai wake.
Komweta Hemed Maneti a.k.a Chiriku
amekuwa akijizolea umaarufu mkubwa katika bendi hiyo kwani mashabiki
wengi wamekuwa wakimkumbuka marehemu baba yake mara anapoimba jukwaani
kwani kwa kiasi kikubwa sauti zinaendana na marehemu baba yake Hemed
Maneti, Bendi ya Vijana Jazz imekuwa ikipata umaarufu siku hadi siku
katika maonyesho yake yanayofanyika kwenye klabu ya Kilwa Road Pub
Ijumaa, Jumamosi wanapiga Jet Lumo na Jumapili kwenye ukumbi wa Vijana
Hall Kinondoni.
Wanamuziki wakongwe waliobaki
kwenye bendi ya vijana Jazz ambao waliwahi kuimba na marehemu Hemed
Maneti ni Shomary Ally,Abdallah Mgonahazeru na Roshy Mselela, Ndoto za
Komweta Hemed ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa na kuipepeprusha vema
bendera ya Tanzania ndani na nje ya mipaka ya TANZANIA ameolewa na ana
mtoto mmoja wa miaka 5 anayeitwa Fahad. Anaongeza kuwa Changamoto za
kazi ya muziki na malezi ni nyingi lakini muhimu ni kujua jinsi gani
utapanga ratiba zako vizuri na kuhakikisha unafanya maandalizi mazuri
kwa ajili ya mtoto na hili halinishindi natimiza majukumu yangu vizuri
kama mama
hata hivyo siku za jumatatu
zinakuwa zina changamoto kubwa sana hasa katika kumwandalia mahitaji
yake kwa ajili ya kwenda shule kwakuwa nakuwa nimechoka na kazi.
Mwanamuziki huyo anasema
mashabiki wa bendi ya vijana wamempokea vizuri sana kusema kweli
anaongeza kuwa “Nashukuru Mungu sana kwa hilo
na hili linajidhihirisha ninapokuwa nafanya shoo zangu…watu hawakai chini mara nyingi wanakuwa wakicheza…”
Anamaliza kwa kusema “Umaarufu wa
marehemu baba yake mzee Hemed Maneti upo na siwezi kuuepuka…lakini kubwa
watu wananipima kutokana na utendaji na ufanisi wangu wa kazi yangu
niwapo jukwaani”.
0 maoni:
Post a Comment