Brazil inatarajiwa kumtangaza
mkufunzi wake mpya katika mkutano na wanahabari siku ya jumanne kufuatia
kujiuzulu kwa kocha wa timu hiyo Luiz Felipe Scolari.
Scolari mwenye umri wa miaka 65 aliiongoza
Brazil katika semi fainali za kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata
kichapo kibaya cha mabao masaba kwa moja dhidi ya mabingwa wa kombe la
Dunia Ujerumani.
Aliyekuwa kocha wa timu hiyo ambaye aliiongoza timu hiyo kati ya mwaka 2006 na 2011 huenda akarejea na kuchukua kazi hiyo.
Wengine wanaopgiwa debe kuchukua kazi hiyo ni
mkufunzi wa kilabu ya Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya Sau Paulo
Muriciy Ramalho na Vanderlei Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza timu
hiyo kutoka mwaka 1998 hadi mwaka 2000.
0 maoni:
Post a Comment