Mtoto: Mourinho amesema hakutaka kumsajili Shaw kwasababu mshahara wake ni mkubwa sana.
Imechapishwa Julai 26, 2014, saa 7:20 mchana
JOSE Mourinho amesema hakuthubutu kutaka
kumsajili Luke Shaw kwasababu mshahara aliohitaji kinda huyo `ungeua
umoja' wa timu kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Shaw mwenye miaka 19, alisaini
Manchester United kwa dau la paundi milioni 30 na inasemekana atakuwa
analipwa mshahara wa paundi laki moja na elfu 20.
Mourinho alisema kiwango hicho ni kikubwa sana kwa klabu yake.
‘Kama unamlipa mshahara mkubwa kijana
mwenye miaka 19 Luke Shaw, tulikuwa tunahitaji nini?, tungekufa' alisema
kocha wa Chelsea. "Tungeua umoja na utulivu wetu katika matumizi ya
hela. Tungeua umoja kwenye vyumba vya kubadilishia nguo".
"Kwasababu unapomlipa zaidi mtoto wa miaka 19-mchezaji mzuri, wa ajabu-siku inayofuata, mimi na (Mkurugenzi wa Chelsea) bwana Mrs
Granovskaia na (mkurugenzi wa ufundi) Michael Emenalo tutagongewa
milango na wachezaji wakisema inawezekanaje tumeichezea klabu mechi 200
na kushinda hili na lile, lakini bwana mdogo anatuzidi mshahara?
Kifaa kipya: Diego Costa, Cesc Fabregas na Filipe Luis wamejiunga na Chelsea majira haya ya kiangazi, sambamba na Didier Drogba.
"Inawezekanaje kijana wa miaka 19
anakuja hapa na kupata hela ambazo hata mimi sipati? ningeua usawa wa
timu na nisingeruhusu hilo kutokea".
'Filipe Luis aliichezea Brazil,
ameshinda makombe ya Ulaya, alicheza nusu fainali ya UEFA, huyu mchezaji
ni bei rahisi kuliko huyu mtoto wa England?
"Sikosoi klabu nyingine kwa kumlipa vile. Lakini kwa klabu yangu, tunaweza kusema ingekuwa mbaya kwetu".
Mourinho alisema inawezekanje Filipe Luis anakuwa na bei rahisi kuliko mtoto wa England, Shaw.
0 maoni:
Post a Comment