Saturday, June 27, 2015


Argentina wameingia Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, COPA AMERICA, baada ya kuitoa Colombia kwa Mikwaju ya Penati 5-4 kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 90 kwenye Mechi ya Robo Fainali iliyochezwa Alfajiri hii.
Katika piga nikupige ya Penati, Timu zote zilifunga Penati zao 3 za kwanza kupitia Lionel Messi, Ezequiel Garay na Ever Banega kwa Argentina huku Colombia wakifunga kupitia James Rodriguez, Radamel Falcao na Juan Cuadrado.

Kwenye Penati ya 4, Muriel akakosa kwa Colombia na Lavezzi kuifungia Argentina na kufanya ngoma iwe 4-3.
Colombia wakafunga Penati yao ya 5 kupitia Cardona na Argentina, wakitakiwa kufunga Penati yao ya 5 ili wasonge, wakakosa Mpigaji akiwa Lucas Biglia na kufanya Bao ziwe 4-4.

Ndipo zikaja nyongeza za Penati moja moja kuamua Mshindi wa papo kwa papo na Colombia kukosa Mpigaji akiwa Zuniga lakini Argentina nao wakakosa ushindi baada ya Marcos Rojo kukosa pia.
Penati iliyofuatia ilipigwa na Colombia lakini Murillo akakosa na akaja Mchezaji mpya wa Boca Juniors ya Argentina, Carlos Tevez, alieanzia Benchi kwenye Mechi hii, na kufunga Penati ya mwisho iliyowapa Argentina ushindi wa Penati 5-4.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog