Na Faustine Ruta, Bukoba
Mh.Mbunge wa Jimbo la Bukoba VijijiniJason Rweikiza ameendelea na Ziara katika Jimbo lake lenye kata 39 kuunga mkono tamko la Rais Jakaya Mrisho Kikwete la kujenga Maabara katika kila Kata kwa ajili ya Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi. Mh. Rweikiza anaendesha Mwenyewe Helkopta akisaidiana na Rubani mwenzake amesema kutokana na Muda kubana imebidi atumie usafiri wa Helkopta ili aweze kukimbizana na muda wa kufanya kazi za Wananchi wa Jimbo lake. Amewaomba Wananchi kuunga mkono jitihada za Rais Kikwete kuchangia ujenzi wa Maabara kwa ajili ya Wanafunzi. Mbali na kuchangi mambo mengine ya Maendelea kila Kata Mh. Rweikiza anachangia kiasi cha Milioni tatu katika Kata 39 kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara, Pia amewataka Wananchi kuunga mkono na kuipigia kura ya ndio Rasimu ya Katiba wakati wa kura za maoni ya Wananchi.
Katika Kata tano za Katoma, Karabagaine, Maruku, Kanyagereko na Kemondo amechangia kiasi cha Millioni 37,750,000/= kwa ajili ya Maabara na Miradi Mingine.
0 maoni:
Post a Comment