Friday, September 5, 2014


Zlatan Ibrahimovic alifunga bao lake la 50 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Estonia

MSHAMBULIAJI wa PSG, Zlatan Ibrahimovic ameweka rekodi ya kuwa mfalme wa ufungaji wa mabao wa wakati wote wa Sweden.
Nyota huyo mwenye miaka 32 alifunga bao safi katika mechi ya kirafiki baina ya Sweden na Estonia na kufikisha mabao 50, akivunja rekodi ya Sven Rydell ambaye kwa mara ya mwisho alifunga mabao 49 dhidi ya Finland mwaka 1932.
Baada ya kuvunja rekodi, Ibrahimovic alivua jezi yake kutoa ujumbe kwa mashabiki. Ilisomeka: 'Ni gjorde det mojligt,' au: 'You made it all possible.' kwa tafsiri isiyo rasmi; "mumefanikisha hili kuwezekana".


Sasa amevunja rekodi ya Rydel aliyeifungia Sweden mabao 49 katika mechi za kimataifa. WAFUNGAJI 10 BORA WA SWEDEN
1. Zlatan Ibrahimovic - Magoli 50 katika mechi 99
2. Sven Rydell - Magoli 49 katika mechi 43
3. Gunnar Nordhal -Magoli 43 katika mechi 33
4. Henrik Larsson - Magoli 37 katika mechi 106
5. Gunnar Gren - Magoli 32 mechi 57
6. Kennet Andersson - Magoli 31 mechi 83
7. Marcus Allback - Magoli 30 mech 74
8. Martin Dahlin - Magoli 29 mechi 60
9. Tomas Brolin - Magoli 27 mechi 47
10. Agne Simonssen - Magoli 27 katika mechi 51


Baada ya kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa mwaka 2001, Ibrahimovic alifunga bao la kwanza katika mechi yake ya kwanza ambayo walishinda mabao 3-0 dhidi ya Azerbaijan katika fainali za kombe la dunia.
Katika michuano ya Ulaya mwaka 2004, wakati huo akiwa Ajax, mshambuliaji huyo alifunga bao la mashindano.
Juhudi zake pia zilimfanya afunge bao dhidi ya Italia na kuongeza ukali wake na hatimaye kusajiliwa na Juventus.
Lakini bao lake kali la kimataifa linalokumbukwa sana alifunga mwaka 2012.
Akiwa tayari ameshafunga mabao matatu dhidi ya England,Ibrahimovic alifunga bao kali akiwa umbali wa mita 35 kwa tiki taka matata na kumuacha Joe Hart akizubaa langoni na alishinda tuzo ya FIFA ya 2013 ya bao bora la mwaka.


Zlatan Ibrahimovic alifunga bao matata dhidi ya Italia na kusajiliwa na Juventus
Baada ya Joe Hart kutoka langoni kuokoa mpira, Zlatan alipiga mpira kwa tikitaka na kufunga goli safi mno

Ibrahimovic alishinda zawadi ya FIFA ya goli bora baada ya kufunga kwa tiki-taka matata dhidi ya England mwaka 2012

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog