Friday, September 5, 2014



Neymar kulia akishangilia bao lake la ushindi dhidi ya  Colombia leo hii Ijumaa walipoichabanga bao 1-0

Neymarakikimbiza na  Juan Zuniga huko Miami

Radamel Falcao kwenye patashika akikabwa
Wakicheza hii Leo huko Sun Life Stadium, Miami ikiwa ni Mechi yao ya kwanza chini ya Kocha Dunga na pia hii ikiwa ni Mechi ya kwanza kwa Neymar kuichezea Brazil tangu avunjwe Mfupa wa Mgongoni na Juan Zuniga wa Colombia kwenye Mechi ya Robo ya Kombe la Dunia Mwezi Julai, Brazil wameifunga Colombia Bao 1-0.
Hadi Mapumziko, Bao zilikuwa 0-0.
Dakika ya 51 Colombia walibaki Mtu 10 baada ya Cuadrado kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu alipopata Kadi ya Njano ya Pili baada kumchezea Rafu Neymar.
Kwenye Kipindi hicho cha pili, Brazil ilimuingiza Mkongwe wao Robinho ambae hajaichezea Nchi hiyo Siku nyingi na Colombia wakamwingiza Straika wao, Falcao, ambae ni Mchezaji mpya wa Manchester United na ambae hakucheza huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia baada ya kuumia Goti.Neymar kwenye patashika dhidi ya wachezaji wa Colombia  Aldo Leao Ramirez

Neymar akifanya yake ndani ya Uwanja wa  Miami Sun Light

Jina mpya wa Aston Villa Carlos Sanchez akichuana na Diego Tardelli

Frikiki murua ya Dakika ya 82 iliyopigwa na Neymar ndio iliwapa Brazil Bao lao moja na la ushindi.
Brazil watacheza Mechi nyingine ya Kirafiki huko Marekani hapo Jumatano dhidi ya Ecuador.

MECHI ZA KIMATAIFA ZA IRAFIKI
RATIBA/MATOKEO:

Ijumaa Septemba 5
Japan 0 vs Uruguay 2
Jumamosi Septemba 6
Brazil 1 Colombia 0
Jumapili Septemba 7
05:00 Chile v Mexico
2145 Serbia v France
Jumatatu Septemba 8
14:00 South Korea v Uruguay
23:00 Saudi Arabia v Australia
Jumatano Septemba 10
03:00 Chile v Haiti
05:00 Brazil v Ecuador
05:00 Mexico v Bolivia

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog