Monday, October 19, 2015

Kamati ya kuisaidia Taifa Stars imetangaza kauli mbiu ya ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza kutumika kuanzia leo hii. 


Kamati hiyo chini ya uenyekiti wa Farouk Baghoza  imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14 Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.
Aidha, Mwenyekiti alitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa nyumbani.  

Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa Kamati Bwana Farough Baghouzah.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog