Wednesday, May 28, 2014


Cardiff City imemsaini Straika wa Manchester United Federico Macheda kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
Macheda, mwenye Miaka 22, anakuwa Mchezaji wa 3 kusainiwa na Cardiff kwa ajili ya Msimu ujao na atahamia bila malipo kuanzia Julai 1 wakati Mkataba wake na Man United utakapoisha. 

Macheda aliwahi kufanya kazi huko Man United chini ya Bosi wa Cardiff, Ole Gunnar Solskjaer, alipokuwa Kocha wa Timu ya Rizevu.
Macheda alijiunga na Timu ya Vijana ya Man United Mwaka 2007 akitokea Lazio na kuwa Mfungaji Bora wa Timu ya Vijana ya chini ya Miaka 18 katika Msimu wake wa kwanza tu Old Trafford kwa kufunga Bao 12 katika Mechi 21.
Mwaka 2009, akiwa na Miaka 17 tu, Macheda aling’ara katika Mechi yake ya kwanza tu na Timu ya Kwanza ya Man United walipokuwa nyuma kwa Bao 2-1 na Aston Villa, Cristiano Ronaldo akasawazisha, na Macheda kupiga Bao la ushindi katika Dakika za Majeruhi na kuisaidia sana Man United kwenye mbio zao za Ubingwa Msimu huo.
Msimu huo, Macheda aliendelea kuonekana mara kadhaa kwenye Timu ya Kwanza na alifunga Bao lake la Pili kwa Man United Sekunde 45 tu baada ya kumbadili Dimitar Berbatov kwenye Mechi na Sunderland.

Msimu huo, Macheda alitunukiwa Tuzo ya Jimmy Murphy ambayo hupewa Mchezaji Bora wa Mwaka toka Chuo cha Soka cha Man United.
Lakini Msimu uliofuatia, Macheda akaanza kuzongwa na Majeruhi ya mara kwa mara na maendeleo yake kuathirika.
Misimu iliyofuatia, Macheda akawa anacheza nje ya Man United kwa Mkopo kwenye Klabu za Sampdoria, Queens Park Rangers, VfB Stuttgart, Doncaster Rovers na Birmingham City, ambako alifunga Bao 10 katika Mechi zake 18.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog