Wednesday, May 28, 2014


UEFA imewafungulia Mashitaka Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone na Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso kwa kuwatuhumu kufanya Utovu wa Nidhamu kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyochezwa Jumamosi iliyopita huko Lisbon, Ureno na Real Madrid kuichapa Atletico Madrid Bao 4-1.
Wote hao wawili wameshitakiwa kwa makosa ya kuvamia Uwanja.
Mara mbili Diego Simeone aliingia Uwanjani wakati wa Dakika za Nyongeza 30 kwenda kumkabili Beki wa Real Raphael Varane na ikabidi azuiwe na Wasaidizi wake.
Pia Simeone alionyesha kukasirishwa na Refa Bjorn Kuipers wa Holland. Nae Xabi Alonso, ambae alikosa kucheza Fainali hiyo kwa sababu alikuwa Kifungoni, alionekana akikimbia nje ya Uwanja baada ya Mechi hiyo.
UEFA imetamka kuwa Kesi za wawili hao zitasikilizwa hapo Julai 17 na wakipatikana na hatia baadhi ya Adhabu zao ni kuzikosa Mechi za UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Vile vile, UEFA imezifungulia Mashitaka Klabu zote mbili, Real Madrid na Atletico Madrid, kwa kuzoa Kadi za Njano 5 kila moja katika Fainali hiyo.
Kwenye Mechi hiyo, Wachezaji 7 wa Atletico na 5 wa Real walipewa Kadi za Njano.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog