Monday, August 31, 2015



Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Oliver Giroud ambaye wengi wamekuwa wakimlaumu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuwa hawezi kutwaa ubingwa akiwa na mshambuliaji huyo pekee, wengi walikuwa wakishinikiza Wenger amsajili Karim Benzema.
August 31 Oliver Giroud amekutana na maswali ya waandishi wa habari kuhusu klabu yake ya Arsenal kuhusishwa kutaka kusajili mshambuliaji mpya. Oliver Giroud ana majibu haya kuhusiana na Arsenal kutaka kumsajili mfaransa mwenzake Karim Benzema na yeye mtazamo wake kuhusu usajili huo.
gun__1412060818_social_giroud
“Ni kweli kila mwaka huwa kuna tetesi za kusajiliwa mshambuliaji mpya, kuna msimu ambao tulimsajili Sanchez, Welbeck na wengine lakini tulikuwa tukizungumza kuhusiana na Suarez, ni kawaida kwa klabu kuna mengi ya kutarajiwa, najua mashabiki wanataka tusajili kwa fedha nyingi”>>> Giroud
“Hilo sio swali ninalopaswa kujibu mimi, kocha anajua vizuri nini anafanya, wakati mwingine hutakiwi usajili tu ili mradi na wakati mwingine kuna kuwa hakuna mchezaji unaye muhitaji, tukiachana na hayo itakuwa vizuri kama Karimu angesajiliwa”>>> Giroud
Olivier-Giroud-Karim-Benzema-601898
Klabu ya Arsenal ya Uingereza ilikuwa ikihusishwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, ambapo Arsenal walikuwa wapo tayari kutoa pound milioni 50 ili kumpata staa huyo kabla ya siku kadhaa nyuma, staa huyo kuthibitisha kuwa hayupo tayari kuondoka Real Madrid.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog