Tuesday, September 1, 2015

August 31 na Septemba 1 ni siku ambazo habari nyingi za michezo barani Ulaya zitatawaliwa na headlines za usajili, kwani dirisha la Usajili kwa Hispania na Ufaransa linaripotiwa kufungwa, lakini nchini Uingereza bado yamebakia masaa kadhaa na wenyewe wafunge, klabu ya West Ham United imetumia vizuri masaa hayo yaliyo salia.
2BDDDE9E00000578-3217951-image-m-58_1441096879912
 West Ham United imefanikiwa kumrudisha kiungo wa kimataifa wa Cameroon aliyekuwa katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania Alex Song, West Ham wanamrudisha kiungo huyo baada ya kuitumikia kwa mkopo timu hiyo msimu uliyomalizika.
2BDDDF2600000578-3217951-image-a-61_1441096924440
Song amerudi tena kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu hiyo akitokea FC Barcelona ya Hispania ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kama ilivyokuwa wakati yupo Arsenal, kwani Song amekuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha FC Barcelona. Pamoja na hayo picha aliyopost mtandaoni akiwa na Emmanuel Adebayor huenda pia mshambuliaji huyo wa Togo yupo njiani kujiunga na klabu hiyo akitokea Tottenham Hotspur.
2BDDB98300000578-3217951-image-a-29_1441092004000
Picha ya Song aliyopost Instagram akiwa na wakala wake pamoja na Adebayor saa kadhaa baada ya kujiunga na West Ham.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog