Tuesday, September 1, 2015


WAKATI Dirisha la Uhamisho likifungwa Usiku huu huko Spain, Real Madrid wamefanikiwa kumnasa Kipa wa Manchester United David De Gea.
Lakini, Real, kwa mujibu wa ripoti za ndani, wanatakiwa wamtoe Kipa wao kutoka Costa Rica, Keylor Navas, kwa Man United na pia kulipa Dau la Pauni Milioni 29.3 kwa Man United na hii inaifanya Man United kufaidika hasa kwa kumuuza Mchezaji ambae amebakisha Mwaka mmoja tu katika Mkataba wake.

Dili hii kwa Man United hii Leo ni ya pili baada ya pia kumchukua Straika Chipukizi wa France, Anthony Martial, kutoka AS Monaco na pengine huenda Jumanne, ambayo ndio Dirisha la Uhamisho linafungwa huko England, wakafanya biashara nyingine kama minong’ono inavyokwenda.

Sakata la De Gea kuhamia Real limedumu kwa kipindi kirefu baada ya Kipa huyo kukataa kusaini Mkataba mpya ulioboreshwa na Meneja wa Man United Louis van Gaal kuamua kutomwita Kikosini katika Mechi zao zote za Msimu huu mpya ulioanza Agosti 8.

Kwenye Mechi zote za Man United Msimu huu, Kipa wa Kimataifa wa Argentina, Sergio Romero, ndio amekuwa akidaka lakini ujio wa Keylor Navas, ambae aling’ara mno wakati wa Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka Jana akidakia Costa Rica, kutaleta ushindani mkubwa.

Real walimnunua Navas toka Levante kwa Dau la Pauni Milioni 7 mara tu baada ya Fainali za Kombe la Dunia kumalizika.

De Gea alinunuliwa na Man United kutoka Atletico Madrid Juni 2011 kwa Dau la Pauni Milioni 17.8 ambalo lilikuwa ni Rekodi kwa Kipa.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog