Sunday, March 9, 2014



Sehemu-ya-Bunge-la-Tanzania-Dodoma1_d83f3.jpg
Ndugu zangu,
Pamoja na kuwa mie si expert wa political science, lakini, kile kidogo ninachokijua naweza kuchangia nanyi. Katika kusoma kwangu Political Science nimesoma pia kwa uchache masuala ya uundwaji ama marekebisho ya Katiba.
- Kwamba marekebisho ya Katiba yanaweza kuwa na sura nyingi. Kuu tatu ni , 1. Yenye kupitishwa na Special Majority 2. Kura za Maoni kwa maana ya referendum, na 3. Bunge la Kawaida.

Hata hivyo, iliyo ya kawaida sana na ambayo yenye kuendana na kuutafuta muafaka ( Consensus) wa kisiasa ni pale panapohitajika mabadiliko husika ya Katiba kuthibitishwa na ' Special Majority''. Hii bila shaka ndio namna ama njia ambayo akina Jaji Warioba na wenzake wanataka kutupitisha.
Njia hii inatoa fursa kwa walio wachache katika kiwango kilichopangwa kuwa na ' Kura ya Turufu' kwa maana ya ' Veto'. Minority veto hapa ni hitaji la uwepo wa ' extraordinary majority' ambapo kwa kawaida huwa ni mbili ya tatu , yaani 2/3.
Katika hili bado, kwa kuangalia Bunge letu maalum la Katiba, kuna wajumbe ambao hawajapata uelewa, kuwa uwingi wa wafuasi wa chama fulani hauna maana ya kuwa wanaweza kupitisha wanayoyataka kwa vile wengine ndani ya Bunge ni wachache.
Hii 2/3 requirement haina maana nyingine bali ni ' Veto Power' ya minority- wachache. Walio wengi bado watahitaji kujenga hoja za kuwashawishi wachache ili wafanikishe 2/3 kwenye maamuzi. Maana, hapa 2/3 inatakiwa itoke kwa wachache. Na wachache nao ni lazima wajenge hoja za ushawishi wapate 2/3 ya walio wengi katika wanachokihitaji.
Hivyo, kwenye 2/3 requirement hakuna kuburuzana bali kushawishiana na kukumbatiana kwa hoja. Vinginevyo, kama utaratibu huo utakiukwa. Na kwa vile ni utaratibu uliopewa ' immunity' ya kisheria . Kuukiuka ni kwamisha mchakato mzima wa mabadiliko ya Katiba, kisheria.
Na kuna mifano ya nchi zinazotumia utaratibu huu kwenye maamuzi yake. Nchi kama Switzerland kwa mfano, Mabadiliko ya Katiba hayawezi kupita bila kuthibitishwa kwa kura za ' Special Majority' ya majimbo madogo kabisa ( cantons) yenye kufanya chini ya asilimia 20 ya watu wote wa Switzerland, hivyo basi, wanatengeneza kinachoitwa pia, a potential vote- kura muhimu au mahsusi.
Na Marekani wamekwenda mbali zaidi, wao wana kinachoitwa ' Three-Fourths'- 3/4. Hitaji la 3/4 ili marekebisho ya Katiba yafanyike katika Marekani lina maana ya majimbo yao 13, ambayo ni madogo sana, na yenye idadi ya watu chini ya asilimia 5 ya Wamarekani wote yanaweza kuzuia mabadiliko ya Katiba katika Marekani.
Hawa nao wana ' minority veto' kwa maana ya ' kura ya turufu' ya wachache. Kwamba ili jambo lipite, kauli zao lazima nazo zisikilizwe!
Ni mchango wangu mdogo kwa leo. Wenye kujua zaidi wanikosoe na watungezee maarifa...

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog